Home Ligi Kuu LIGI KUU BARA KADI 600 ZATOLEWA…MGUNDA AMKANA KANOUTE…”NAMUONYA SANA HASIKII

LIGI KUU BARA KADI 600 ZATOLEWA…MGUNDA AMKANA KANOUTE…”NAMUONYA SANA HASIKII

LIGI KUU BARA KADI 630 ZATOLEWA...MGUNDA AMKANA KANOUTE...

LIGI Kuu Bara kwa imesimama kupisha mechi za kimataifa za timu ya taifa, Taifa Stars dhidi ya Uganda The Cranes sambamba na mechi za robo fainali ya ASFC zitakazopigwa mapema mwezi ujao, lakini hadi ligi hiyo ikikamilisha mechi 199, kadi zimetembea sana.

Wakati tukisubiri kushuhudia mechi hizo za kimataifa, kwenye Ligi Kuu hadi sasa kila timu imejiwekea rekodi zake tamu na mbaya na kati ya hizo ni kadi za njano na nyekundu ambazo msimu huu zimetolewa kwa wingi.

Ukitoa Simba na Yanga zilizocheza mechi 24 na kubakiza sita tu ili kumaliza ligi, timu nyingine 14 zimecheza michezo 25 kila moja na zimebakiwa na mechi tano tano kumaliza msimu.

Katika mechi zote hizo, zimetolewa kadi nyekundu na njano zisizopungua 630 na hapa ni takwimu za kadi hizo kwa kuzingatia timu na wachezaji wake.

NJANO

Hadi sasa zimetoka kadi za njano 611 zikienda kwa timu zote 16 za Ligi Kuu ambapo Dodoma Jiji ndio vinara wa kucheza madhambi wakiwa nazo 57 wakifuatiwa na Namungo yenye 50, huku Azam, Simba, Singida Big Stars na Ihefu zikifuatia zote zikiwa na kadi za njano 42.

Kagera Sugar ndiyo timu yenye kadi za njano chache ikiwa nazo 27, KMC ikiwa na 28 na Yanga ikiwa na 29 huku nyingine zote zikiwa na kadi kuanzia 30 kwenda juu.

Kiungo Mmali wa Simba, Sadio Kanoute ndiye anaongoza kwa kuwa na kadi nyingi za njano akiwa nazo 10, akifuatiwa na Salmin Hoza wa Dodoma mwenye tisa, Juma Nyosso wa Ihefu ana nane wakati Mtenja Albano wa Coastal, Charles Ilamfya wa Mtibwa, Hassan Nassoro na George Sangija wa Mbeya City kila mmoja anazo saba.

UMEME

Hadi sasa zimetolewa kadi nyekundu 22 ambazo zimeenda kwa wachezaji wa timu 10 kati ya 16 za Ligi Kuu ambazo ni Polisi Tanzania, Mtibwa Sugar, Geita Gold, Namungo, Tanzania Prisons, Dodoma Jiji, Mbeya City na Azam FC, Simba, Kagera Sugar.

Polisi ndiyo timu yenye kadi nyingi nyekundu ikiwa nazo tano, ikifutiwa na Mtibwa yenye nne, huku Geita, Namungo, Azam, Prisons, Dodoma Jiji kila timu ikiwa nazo mbili na Simba, Kagera na Mbeya City wakiwa nazo moja moja.

Nahodha wa Polisi, Mohamed Mmanga ni mchezaji pekee aliyepata kadi nyekundu mara mbili huku wengine wakiwa nazo moja moja tu.

WASIKIE WENYEWE

Mshambuliaji wa Mtibwa Sugar, Charles Ilamfya ambaye ni miongoni mwa vinara wa kadi za njano akiwa nazo saba alisema hapendi kufanya madhambi kwa makusudi lakini inatokea kutokana na ari ya mchezo inavyokuwa.

“Hakuna anayependa kumfanyia faulo mwenzake, inatokoea katika kupambania timu yako, kuna muda unahisi uko sahihi lakini kumbe umekosea na wakati mwingine presha na hali ya mchezo husika huchangia mtu kupata kadi,” alisema Ilamfya.

Kocha Msaidizi wa Simba, Juma Mgunda ambaye kiungo wake Sadio Kanoute ndiye anaoongoza kwa kuwa na kadi nyingi za njano (10), alisema mara nyingi anamuonya mchezaji huyo na wengine kutocheza madhambi lakini wakifika uwanjani mambo yanabadilika.

“Nadhani shida sio makocha bali ni aina ya uchezaji wa mchezaji husika, sisi huwa tunaongea na wachezaji wetu tukiwahamasisha wacheze kwa nidhamu lakini mechi ikianza mambo yanabadilika, nimecheza mpira na najua kuna faulo zinakuwa za makusudi na nyingine hutokea tu lakini pia zipo za kujilinda zaidi hivyo kwa mchezaji kama kiungo mkabaji sio jambo la kushangaa akipata kadi hiyo hutokana na aina ya uchezaji wake,” alisema Mgunda.

Mkufunzi wa Waamuzi wa CAF, Leslie Liunda alisema mchezaji, au mhusika yeyote wa mchezo wa soka anayekiuka sheria za mchezo huo ni yake yake kuadhibiwa kwa kadi.

SOMA NA HII  KWA TAKWIMU HIZI TU....HUYU MUDATHIRI ATAFUNGA SANA MSIMU HUU....