Home Michezo MAMA SAMIA AWAMWAGA MPUNGA…MIL 500 MEZANI…TAIFA STARS IKIFUZU AFCON

MAMA SAMIA AWAMWAGA MPUNGA…MIL 500 MEZANI…TAIFA STARS IKIFUZU AFCON

MAMA SAMIA AWAMWAGA MPUNGA...MIL 500 MEZANI...TAIFA STARS IKIFUZU AFCON

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Pindi Chana amesema Serikali itatoa Sh500 milioni kwa timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ ikiwa itafuzu kucheza fainali za mashindano ya Afcon 2023.

Dk Chana amesema Serikali imejipanga vyema kuwaunga mkono wachezaji wa timu ya Taifa ili kuhakikisha wanafanya vizuri.

Amesema kuwa wachezaji wamejipanga vilivyo hivyo serikali haina budi kutoa ushirikiano kwa hali na mali.

“Naibu Waziri Hamis Mwijuma atakwenda kutuwakilisha Wizara ya Michezo kwa ujumla na ataelekea Misri kuungana na wachezaji na mashabiki watakaoweza kuhudhuria katika mchezo huo dhidi ya Uganda,”

“Nawaomba Mashabiki wafike kwa wingi hata siku ya mechi ya marudiano kwani wao ni wachezaji namba 12 na uwepo wao ni faraja kwa wachezaji wetu.”

Wadau wa michezo walioweza kufika katika mkutano huo wamesema kuwa, Serikali imefanya vyema kuwaunga mkono timu ya Taifa kwani ilikuwa imesahaulika.

Wamesema kuwa viongozi wameonyesha kujali hali inayowapa morali mashabiki pia wachezaji kucheza na kupata matokeo mazuri huko Misri na hata uwanja wa nyumbani.

Taifa Stars imeshafika nchini Misri tayari kwaajili mchezo dhidi ya Uganda The Crane mchezo utakaochezwa katika uwanja uliopo mji wa Ismailia wa Machi 24.

SOMA NA HII  SAKATA LA MANARA NA TFF...KWA MARA YA KWANZA KARIA AFUNGUKA ...ATUPA KIJEMBE KWA UBINGWA WA YANGA...