Home Habari za michezo MOHMMED HUSSEIN “TSHABALALA” NA KIBU DENNIS…WAPIGWA OUT SIMBA

MOHMMED HUSSEIN “TSHABALALA” NA KIBU DENNIS…WAPIGWA OUT SIMBA

CHAMA ASHTUSHWA KAPOMBE NA TSHABALALA KUACHWA STARS WADAU WAZUNGUMZA

Wachezaji tegemeo ndani ya kikosi cha Simba, Kibu Denis na Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ wanatarajiwa kuukosa mchezo dhidi ya Raja Casablanca.

Simba ambayo ipo nafasi ya pili katika Kundi C la Ligi ya Mabingwa Afrika, itavaana dhidi ya Raja Casablanca ukiwa ni mchezo wa mwisho wa hatua hiyo utakaopigwa ugenini huko Morocco.

Taarifa ambazo imezipata Spoti Xtra, kutoka ndani ya Benchi la Ufundi la Simba, nyota hao wataukosa mchezo huo kutokana na adhabu ya kadi za njano ambazo wamezipata katika michezo iliyopita.

Mtoa taarifa huyo alisema kadi walizopata nyota hao katika mchezo uliopita dhidi ya Horoya AC wakati Simba ikishinda 7-0, ndiyo zimewafanya waukose mchezo ujao.

Aliongeza kuwa, kocha mkuu wa timu hiyo, Roberto Oliveira ‘Robertinho’ ameanza maandalizi ya kuwatengeneza wachezaji wengine watakaokuja kuchukua nafasi zao mara baada ya kikosi hicho kuingia kambini Jumatano.

“Tukijiandaa na mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, tunatarajia kuwakosa wachezaji wetu muhimu wawili ambao ni tegemeo katika kikosi cha kwanza.

“Kukosekana kwao ni pengo kubwa, lakini kocha atafanya maandalizi ya kutosha mazoezini ili kuhakikisha anawapata wengine watakaocheza na kuziba nafasi zao,” alisema mtoa taarifa huyo.

SOMA NA HII  VITUO VYA TIKETI MECHI YA SIMBA SC VS HOROYA AC...TIKETI ZA MZUNGUKO BUKU 3 TU...TWENZETU KWA MKAPA