Home Habari za michezo MTAALAMU WA YANGA SC…ATEKWA NA WALIBERIA…APATIWA MISHENI YA SIRI

MTAALAMU WA YANGA SC…ATEKWA NA WALIBERIA…APATIWA MISHENI YA SIRI

Habari za Yanga SC

UBORA iliyonayo Yanga kwa sasa unavuma sio hapa Tanzania tu, bali hadi katika mataifa mengine ya Afrika na sasa Shirikisho la Soka Liberia limekubali pigo moja walilopigwa mapema na Yanga na wakijisalimisha kumuomba mtaalamu mmoja wa klabu hiyo ili akawapigie deiwaka.

Liberia imewaomba Yanga kuwapatia kwa muda mtaalamu wa kuchambua mikanda ya video ya mechi za wapinzani, Mtunisia Khalil Ben Youssef kwenda kufanya kazi katika kikosi cha taifa hilo ambalo juzi kati liliiduwaza Afrika Kusini kwa kupindua meza ugenini kwa kutoka nyuma ya mabao 2-0 na kumaliza mechi kwa sare ya 2-2.

Liberia ilikuwa katika hesabu za kumchukua Youssef mapema, lakini wakazembea kidogo na Yanga wamchukua fasta mtaalam huyo hatua iliyowafanya shirikisho hilo kuwasilisha maombi maalum.

Youssef sasa kwa ruhusa ya Yanga atakuwa anakwenda Liberia wakati wa mechi za kalenda za mechi za kimataifa kuungana na benchi la timu hiyo kisha mechi hizo zinaposimama atarejea haraka kuendelea na majukumu yake kwa ‘Wananchi‘.

Mtaalamu huyo alikuwa katika benchi la Liberia wakati wakiilazimisha sare Afrika Kusini ya mabao 2-2 mchezo uliochezwa nchini Afrika Kusini Machi 24 ambapo ataendelea na majukumu yake katika mchezo wa marudiano utakapigwa kesho nchini Liberia.

“Huyu ilikuwa aende Liberia lakini wakati tunamalizana naye tu, kesho yake akaanza kutafutwa na shirikisho la kule Liberia ili wamtumie mkataba wakawa wameshachelewa,” alisema mmoja wa mabosi wa juu wa Yanga aliyefafanua zaidi;

“Walituomba na bahati nzuri hata yeye Youssef alishatuambia tukaona haina shida kwa kuwa ratiba ambayo wameiomba haitakuwa na muingiliano na majukumu ya klabu yetu, kahiyo atakuwa anakwenda kwa muda maalumu.”

SOKA LA BONGO linafahamu kuwa Yanga imempa jukumu la siri mtaalamu huyo kuangalia mastaa wapya wa maana katika mechi atakazokuwa anakwenda katika kusuka kikosi chao imara kwa msimu ujao.

Youssef amekuwa pia akiwasaidia makocha wa Yanga kutoa mapungufu mbalimbali ya wachezaji wa timu hiyo kiufundi kupitia mechi ambazo Yanga inacheza kazi ambayo ameanza kuifanya tangu atue nchini.

Yanga inajiandaa na mechi ya marudiano ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya TP Mazembe itakayopigwa Jumapili jijini Lubumbashi, DR Congo ikiwa tyari ina tiketi ya kucheza robo fainali ya michuano hiyo pamoja na US Monastir ya Tunisia itakayokuwa nyumbani kucheza na Real Bamako

SOMA NA HII  FARID MUSSA ATOBOA SIRI GOLI ALILOWAPIGA MAZEMBE...AMEZUNGUMZA HAYA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here