Home Habari za michezo NABI SIWAOGOPI WAARABU…KUWENI WAPOLE NIWANYOOSHE…TUMEPATA SIRI ZAO

NABI SIWAOGOPI WAARABU…KUWENI WAPOLE NIWANYOOSHE…TUMEPATA SIRI ZAO

NABI: SIWAOGOPI WAARABU...KUWENI WAPOLE NIWANYOOSHE...TUMEPATA SIRI ZAO

Kocha wa Yanga, Profesa Nasreddine Nabi amesema Hawaogopi Monastir, japo waliwafunga kwao na wao wana uwezo wa kuwafunga hapa na wanaendelea kufanyia kazi Mipango kuhakikisha wanashinda mchezo huo na kufuzu.

“Itakuwa mechi ngumu kwetu lakini tayari tumejua baadhi ya mipango ya wapinzani wetu hivyo tunaweza kuanzia hapo kuhakikisha tunashinda.

“Siwezi kuweka kila kitu hadharani lakini jua tunachohitaji ni ushindi tu na tuna uhakika na hilo kutokana na mechi ilivyo na vitu ambavyo tunavyo hadi sasa,” alisema Nabi ambaye anaamini kwa walivyojipanga, Yanga inatinga robo fainali.

Yanga wataikaribisha US Monastir katika mchezo wa mzunguko wa tano hatua ya Makundi Kombe la Shirikisho Afrika.

SOMA NA HII  MASHABIKI WA MBEYA CITY WACHARUKA..."KOCHA ANAZINGUA SANA...TIMU HAINA UWEZO KABISA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here