Home Habari za michezo PAMOJA NA KUFUZU ROBO FAINAL…SHAFFI DAUDA AZIKANDIA SIMBA NA YANGA…ADAIA HAZINA MSAADA...

PAMOJA NA KUFUZU ROBO FAINAL…SHAFFI DAUDA AZIKANDIA SIMBA NA YANGA…ADAIA HAZINA MSAADA NA NCHI…

Habari za Yanga

Wakati Simba na Yanga zikitinga hatua ya Robo Fainali Michuano ya CAF na kupongezwa kila kona na wadau wa Soka nchini.

Mchambuzi wa Michezo Shaffi Dauda yeye kwa upande wake amesema kuwa licha ya vilabu hivyo kufanya vyema lakini havina msada kwa mpira wa Tanzania na hasa Timu ya Taifa.

Akizungumza Shaffih amesema;

“Simba na Yanga haziko kwa ajili ya kuusaidia Mpira wa Tanzania. Hivi sasa timu zao zipo Robo Fainali lakini Mchango wa wachezaji watanzania mpaka kufika hapo ni mdogo.Kuna haja ya kupunguza idadi ya Wachezaji wa Kigeni mpaka kufikia watano ili kujenga timu imara ya Taifa”

Timu ya Taifa ya Tanzania ipo nchini Misri ikijiandaa na mchezo wa kufuzu AFCON 2023 dhidi ya Uganda Machi 24.

SOMA NA HII  SHOW ZA PESA NDANI YA EXPPANSE CASINO ZIMERUDI KWA NGUVU....