Home Habari za michezo POLISI TANZANIA WAOGESHWA MANOTI…MWINYI ZAHERA ASHANGAZWA!!

POLISI TANZANIA WAOGESHWA MANOTI…MWINYI ZAHERA ASHANGAZWA!!

 wachezaji kupambana na kutupatia ushindi ndio maana tumeweka bonasi hiyo ili kuwapa motisha na hali ya upambanaji zaidi. Kwa upande wetu viongozi tunaendelea kuihudumia timu na kuhakikisha wachezaji wetu wanafanya kazi katika mazingira rafiki na mengine tumewaachia benchi la ufundi,

Kikosi cha Polisi Tanzania kimeendelea kujinoa kuhakikisha kinajinasua mkiani mwa Ligi Kuu, huku mastaa wa timu hiyo wakiwekewa mamilioni mezani ili wapambane na kuipusha ishuke daraja.

Polisi inaburuza mkia kwenye ligi ikiwa na pointi 19 na imebakiza mechi tano tu kumaliza msimu jambo ambalo ni hatari, kwani isipokaza buti itashuka daraja jambo lililowastua viongozi wa timu hiyo na kuamua kuwapa bonasi ya karibu Sh100 Milioni wachezaji kama wataweza kuibakiza ligi kuu.

Katika moja ya vikao vya ndani kati ya viongozi na wachezaji, mastaa wa kikosi hicho waliambiwa kama wataweza kuibakisha timu Ligi Kuu watapewa bonasi ambayo Mwanaspoti imeinyaka kuwa ni wastani wa Sh3 Milioni kwa kila mchezaji.

Bonasi hiyo itawajumlisha viongozi wengine wa moja kwa moja kwenye timu ikiwemo benchi la ufundi linalongozwa na Kocha Mkongomani, Mwinyi Zahera.

Akizungumza na Soka la bongo, moja ya kiongozi wa juu wa timu hiyo (jina tunalo), amesema wamefanya hivyo ili kuongeza morali kwa wachezaji.

“Kwa hali tuliyonayo kwa sasa kinachoweza kutuokoa zaidi ni wachezaji kupambana na kutupatia ushindi ndio maana tumeweka bonasi hiyo ili kuwapa motisha na hali ya upambanaji zaidi.

Kwa upande wetu viongozi tunaendelea kuihudumia timu na kuhakikisha wachezaji wetu wanafanya kazi katika mazingira rafiki na mengine tumewaachia benchi la ufundi,” alisema.

Polisi imecheza mechi 25, ikishinda nne, sare saba na kupoteza 14 ikiwa na pointi 19 na kwenye mechi tano ilizosalia itavaana na Singida Big Stars, Ihefu, Mtibwa Sugar, Simba na Azam.

SOMA NA HII  JOB:- MAMELOD WAMESHAJAA KWENYE MFUMO....5G ITAHUSIKA TU....