Home Habari za Simba RAISI WA SIMBA MO DEWJI…KILA SIKU UNALALAMIKA HASARA… KAMA UMEOCHOKA ACHIA TIMU

RAISI WA SIMBA MO DEWJI…KILA SIKU UNALALAMIKA HASARA… KAMA UMEOCHOKA ACHIA TIMU

Habari za Simba SC

Wakati mahojiano ya Rais wa heshima wa Klabu ya Simba SC, na mdhamini wa Klabu hiyo Mohammed Dewji yakizidi kuwaacha watu na maswali, baadhi ya wapenda soka nchini wameendelea kutoa maoni yao kuhusiana na mahojiano hayo aliyofanya na kituo cha Global TV.

Akinukuliwa Mo alisema tangu aanze kuwekeza pesa zake ndani ya Klabu hiyo hajapata faida zaidi ya hasara.

Sasa Mchambuzi wa michezo kutoka kituo cha Wasafi FM, George Job amekuja na maoni yake kuhusiana na kauli za tajiti huyo wa Simba.
Akizungumza kupitia kipindi cha Sports Arena George anasema;

“Kila mmoja anaelewa kwamba kwenye mpira kuna hasara na yeye (Mo Dewji) anajua hilo. Hamna kitu kinachonikwaza kama kila siku utuambie unapata hasara. Kila anapoibuka ni mada ya kupata hasara. Kama amechoka atoke nje ya timu.”

SOMA NA HII  KIBU DENIS AVUNJA REKODI HII YA KICHUYA...KATIKA MECHI YA SIMBA NA YANGA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here