Home Habari za michezo RASMI….SIMBA KUKUTANA NA HAWA ROBO FAINAL CAF…SHUGHULI KUANZA UPYAA…

RASMI….SIMBA KUKUTANA NA HAWA ROBO FAINAL CAF…SHUGHULI KUANZA UPYAA…

Habari za Simba SC

Simba kwa sasa wanakula kuku kwa mrija ikiwa ni baada ya timu hiyo kutinga hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika lakini kama unadhani kazi imekwisha basi fahamu bado kabisa.

Kazi ambayo Simba wanayo kwa sasa ni kumfahamu mpinzani gani ambaye watapangiwa kwenye hatua ijayo ya michuano hiyo ambayo inasimamiwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) ambapo kwa mujibu wa rekodi ni lazima waangukie kwa kigogo mmoja katika hatua hiyo inayofuata.

Simba walitinga hatua hiyo ya robo baada ya kuwafanya kitu mbaya Horoya AC ya Guinea kwa kuwachapa mabao 7-0 Jumamosi iliyopita katika Uwanja wa Mkapa, Dar na kuwafanya kujihakikishia kumaliza nafasi ya pili kwenye Kundi lao C nyuma ya Raja Casabalanca.

Simba wamefuzu hatua hiyo baada ya kufikisha alama tisa nyuma ya Raja wenye 13 huku Horoya wakiwa nazo nne na Vipers wakiwa wanaburuza kundi wakiwa na alama mbili. Mechi yao ijayo Simba watacheza dhidi ya Raja ambao utakuwa wa kufunga hesabu.

Kwa kushika nafasi ya pili kwenye kundi lake kwa mujibu wa sheria za CAF ni kwamba mshindi wa pili wa kundi husika basi anatarajiwa kukutana na mshindi wa kwanza katika makundi mengine.

Vigogo ambao anatarajia kukutana nao Simba kwenye hatua hiyo ya robo ni Wydad Casablanca au JS Kabyle kutoka Kundi A ambao wote wana pointi 10, hivyo yanasubiriwa matokeo ya mchezo wa mwisho baina ya timu hizo atayemaliza katika nafasi ya kwanza basi atakuwa na nafasi kukutana na Simba.

Kwa upande wa kundi B mpaka sasa Mamelodi Sundowns ndiye kinara akiwa na pointi zake 11 huku Al Hilal wakiwa na pointi 10 na Al Ahly wakiwa na pointi 7, hivyo hapo Simba anatarajiwa kukutana na yoyote kati ya Al Hilal au Mamelodi kwa ambaye ataongoza kundi hilo.

Kwa upande wa Kundi D, Simba anatarajiwa kukutana na Espérance Tunis wenye pointi 10 au CR Belouzidad wenye pointi 9, hivyo yoyote ambaye ataongoza kundi huenda akakutana na Simba.

Mfumo ambao utatumika kupata timu zitakazokutana katika robo fainali hufanyika kwa kuchukuliwa timu nne ambazo zimeongoza kila kundi kisha kufanyika droo na timu nne zilizoshika nafasi ya pili kwa kila kundi kisha kupatikana mechi za robo fainali.

SOMA NA HII  A-Z KILICHOWAMALIZA SIMBA MBELE YA AL AHLY JANA....WAARABU WAONDOKA NA JINA LA KIBU...