Home Michezo SABABU ZA FEISAL SALUM “FEI TOTO” KUITWA STARS…”YUPO FIT SANA LICHA YA...

SABABU ZA FEISAL SALUM “FEI TOTO” KUITWA STARS…”YUPO FIT SANA LICHA YA MATATIZO…MCHEZAJI MZURI ATATUSAIDIA

SABABU ZA FEISAL SALUM

Kocha Msaidizi wa Taifa, Hemed Morocco, ametaja sababu ya kumuita Kiungo Mshambuliaji Feisal Salum Abdallah ‘Fei Toto’ kwenye timu ya taifa kuwa ni kutokana na umri wake mdogo.

Morocco amesema kikubwa walichokizingatia ni kujiridhisha kuwa anafanya mazoezi ukiachilia mbali matatizo baina yake na klabu yake ya Yanga SC.

“Ni Mchezaji ambaye anaonekana anafanya mazoezi yuko vizuri na hiki ni kitu cha kupambania Nchi, ukiwa mchezaji mzuri hata kama una matatizo tutakuita, falsafa yetu imeona atatusaidia Feisal ni mdogo na tunapenda Wachezaji wadogo hata kama hawapo katika mechi za ushindani muhimu wanafanya mazoezi tumejiridhisha, ndio maana tumemchagua,” alisema Morocco.

SOMA NA HII  MAYELE HAONEKANI KAMBINI...APIGWA CHINI YANGA...ISHU NZIMA IKO HIVI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here