Home Michezo SIMBA NA YANGA HAKUNA MBABE…TAMBO ZIMEISHA MIDOMONI

SIMBA NA YANGA HAKUNA MBABE…TAMBO ZIMEISHA MIDOMONI

SIMBA NA YANGA HAKUNA MBABE...TAMBO ZIMEISHA MIDOMONI

Mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania (Serengeti Lite Women’s Premier League #SLWPL) kati ya Yanga Princes na Simba Queens umemalizika katika Dimba la Uhuru jijini Dar es Salaam kwa timu hizo kutoshana nguvu baada ya kutoa sare ya bao 1-1.

Katika mchezo huo ambao Yanga Princess walikuwa wenyeji, Simba Queens ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao kuinako dakika ya 30 kupitia kwa Jentrix Shikangwa dakika ya 35 ya kipindi cha kwanza, bao lililodumu mpaka kipindi cha pili kabla ya Yanga kusawadhisha dakika ya 75 kupitia kwa Wogu Chioma.

Kwa matokeo hayo, Simba wakiwa na alama 27 wameshuka kutoka nafasi ya kwanza mpaka ya tatu kufuatia ushindi wa Foutain Gate dhidi ya Mkwawa ambapo Fountain wamepanda mpaka nafasi ya kwanza wakifikisha alama 29, na ya pili ikishikwa na JKT wenye alama 28.
Matokeo mengine; Baobab 0-3 JKT

Mkwawa 0-2 Foutain Gate
Wafungaji;
Priviledge Mupeti
Neema Paul
Msimamo wa Ligi;

Fountain Gate – 29 JKT – 28
Simba Queens – 27
Yanga Princes – 22.

SOMA NA HII  KIBU DENIS KUANDIKA HISTORIA MPYA MSIMBAZI...MASHABIKI WAPEWA NENO 'KUNTU' NA MABOSI SIMBA...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here