Home Habari za michezo SIMBA WAZIDI KUIFUNIKA YANGA KWA PESA BONGO…DILI JIPYA LA MIL 500 HILI...

SIMBA WAZIDI KUIFUNIKA YANGA KWA PESA BONGO…DILI JIPYA LA MIL 500 HILI HAPA…

Habari za Simba SC

Kampuni ya MobiAd Afrika leo imetangaza kudhamini Timu ya Vijana ya Simba kwa mkataba wenye thamani ya Tsh. Milioni 500 kwa miaka miwili ambao unalenga kukuza Soka la Vijana.

CEO wa MobiAd Africa, Rumisho Shikonyi amenukuliwa akisema “Tumeona hii ni fursa kuungana kwenye hii safari, tunatangaza udhamini kwa Timu ya Vijana ya Simba Sports Club kwa mkataba wenye thamani ya Tsh. Milioni 500 kwa miaka miwili, tunaamini mpira wa miguu ni sehemu ya suluhisho la ajira kwa Vijana, Simba ni Timu kubwa Afrika na inazidi kuwa kubwa hivyo ni vizuri kuandaa Vijana ambao watachukua nafasi ya hawa wa sasa”

CEO wa Simba, Imani Kajula amesema “Soka la Vijana ni muhimu sana ili uwe na Timu ya Vijana iliyo bora lazima iwezeshwe, kama ilivyo kwa Wachezaji wengine kama Mohamed Hussein kutoka kwa Timu ya Vijana”

“Simba inakwenda mbele kutambua vipaji, kuvichukua na kuviendeleza na kuweza kutengeneza Timu yenye vipaji vikubwa sana, tunaamini Simba imara yenye vipaji haitaisaidia Simba pekee bali hata Taifa letu”

Kwa upande wake , Ahmed Ally amesema ““Tunakwenda kubadili taswira ya mpira wa Vijana, uzuri tunajua tunachofanya,  ndio tumetoa Vinana wengi ambao wanafanya vizuri kwenye Timu za Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza, tunao Watu ambao wanajua namna ya kukuza Soka la Vijana

SOMA NA HII  BOCCO NA MUGALU KUONGOZA JESHI LA SIMBA SC VS TANZANIA POLISI