Home Habari za michezo TANZANIA 0-1 UGANDA TAIFA STARS WALA KICHAPO…NDOTO ZA AFCON BYE BYE…MICHO AONYESHA...

TANZANIA 0-1 UGANDA TAIFA STARS WALA KICHAPO…NDOTO ZA AFCON BYE BYE…MICHO AONYESHA UBABE

TANZANIA 0-1 UGANDA TAIFA STARS WALA KICHAPO...NDOTO ZA AFCON BYE BYE...MICHO AONYESHA UBABE

MCHEZO wa kufuzu fainali za Mataifa Afrika ya (AFCON) kati timu ya taifa ‘Taifa Stars’ dhidi ya Uganda ‘The Cranes’ zimetamatika kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa kwa wenyeji kukubali kichapo cha bao 1-0.

ZIFUATAZO NI DONDOO KADHAA ZA MCHEZO HUU

Huu ni mchezo wa pili kwa kocha, Adel Amrouche tangu ateuliwe kukiongoza kikosi cha Stars Machi 4 mwaka huu ambapo kati ya hiyo ameshinda mechi moja tu ya bao 1-0 dhidi ya Uganda na kupoteza pia 1-0 na Uganda.

Tangu kutimuliwa kwa, Kim Poulsen Agosti 29 mwaka jana, Stars ilikuwa chini ya kocha wa muda Mzambia, Hanour Janza ambaye alirudi kwao baada ya kupata dili la kuwa Mkurugenzi wa Ufundi wa Klabu ya Zesco.

Mara ya mwisho kwa Stars kucheza AFCON ilikuwa ni mwaka 2019 kule nchini Misri ikiwa chini ya Kocha Mkuu, Mnigeria, Emmanuel Amunike baada ya kukaa kwa muda wa miaka 39.

Mwaka 1980 ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Stars kushiriki michuano hiyo ikifundishwa na Mpolandi, Slawomir Wolk katika fainali hizo zilizofanyika Nigeria.

Katika michezo 21 iliyopita baina ya timu hizi zilipokutana Stars imeshinda minne, sare minne na kupoteza 13.

Stars katika michezo 10 ikiwa mwenyeji kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa dhidi ya Uganda imeshinda mmoja, sare miwili na kuchezea kichapo mara saba.

Tanzania na Uganda zimekutana mara 12 katika michezo ya kufuzu AFCON ambapo Stars imeshinda mitatu, sare minne na kupoteza minne.

Uganda mara ya mwisho kwake kushinda mbali na leo katika michezo yake sita ikiwa ugenini dhidi ya Tanzania katika michuano ya AFCON ilikuwa ni ushindi wa bao 1-0 ambao iliupata mwaka 1984.

Huu ni mchezo wa 27 kwenye mashindano yote kwa kocha wa Uganda, Milutin Sredojevic ‘Micho’ tangu alipoteuliwa Julai 27, 2021 akichukua nafasi ya Johnathan McKinstry.

Katika michezo hiyo ambayo pia na ya kirafiki Micho ameshinda minane, sare 11 na kupoteza minane.

Kwa matokeo haya Katika kundi ‘F’ Stars inasalia nafasi ya pili na pointi nne nyuma ya vinara Algeria ambayo tayari imefuzu baada ya kufikisha jumla ya pointi 12 kufuatia timu zote kucheza michezo minne.

Kwa upande wa Uganda inafikisha pia pointi nne huku Niger ikiburuza mkia ikiwa na pointi mbili.

SOMA NA HII  KOCHA MKUU WA TANZANIA PRISONS...MOHAMED ABDALLAH 'Bares'...AZUNGUMZA NA MASHABIKI