Home Habari za michezo WACHEZAJI TP MAZEMBE WAKATWA MISHAHARA…KWA KUSHINDWA KUVUKA MAKUNDI

WACHEZAJI TP MAZEMBE WAKATWA MISHAHARA…KWA KUSHINDWA KUVUKA MAKUNDI

WACHEZAJI TP MAZEMBE WAKATWA MISHAHARA...KWA KUSHINDWA KUVUKA MAKUNDI

Asiyefanya kazi na asile. Ndicho ambacho Bilionea Moise Katumbi ameamua kwa mastaa wake, watakatwa mishahara yao kwa asilimia 25 kwa Kushindwa kuvuka hatua ya Makundi katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Roho mbaya hii sio ya ghafla ghafla tu. hivi ndivyo ilivyo kwa katika mpangilio wa mishahara ya mastaa wa Mazembe kwa mujibu wa mikataba yao.

Watalazimika kukatwa robo ya mishahara yao kama wakishindwa kuivusha Makundi timu yao katika michuano ya Afrika, na jana rasmi wamejitoa katika kinyanganyiro cha kufuzu kwa hatua ya Robo Fainali Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kukubali kichapo cha magoli 2-1 mbele ya Real Bamako.

SOMA NA HII  SIKU 7 KABLA YA KUKIPIGA NA SIMBA DAR....YANGA KUIVAA SINGIDA FG KININJA KESHO,...