Home Habari za michezo WAKILI SAIMON:- WAMEFANIKIWA KUMUHARIBIA FEI TOTO MAISHA YAKE…YANGA IMEPOTEZA MCHEZAJI…

WAKILI SAIMON:- WAMEFANIKIWA KUMUHARIBIA FEI TOTO MAISHA YAKE…YANGA IMEPOTEZA MCHEZAJI…

Habari za Yanga SC

Mwanasheria wa Klabu ya Yanga, Wakili Patrick Simon amesema kuwa waliomrubuni mchezaji wao Feisal Salum ‘Fei Toto’ kutaka kuvunja mkataba wamefanikiwa kumharibia taaluma yake na maisha yake ya mbeleni.

Kauli hiyo ya Patrick inakuja ikiwa ni baada ya kiungo huyo kutoka Zanzibar amegonga mwamba kwa mara ya pili, mbele ya Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka nchini Tanzania ‘TFF’.

Kutoka kwenye ukurasa wa Twitter ya wakili Simon, ameandika;

“Mtazamo Wangu:

– Yanga imepoteza mchezaji wake. – Kijana kapoteza nafasi ya kucheza mpira. – Aliyenyuma ya kijana kafanikiwa kumuharibia maisha. – Familia ya Kijana imenufaika kimaisha. – Wanasheria wa Kijana wamejitengenezea pesa. – Waandishi wamefanikiwa kutengeneza Content.”

Feisal aliomba kurejewa kwa maamuzi ya shauri lake dhidi ya Yanga, lakini bado Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ikaendelea kusimamia msimamo wake wa kumtambua kama Mchezaji halali wa Klabu hiyo ya Jangwani.

Feisal alitangaza hadharani kuvunja mkataba na Young Africans mwishoni mwa mwaka 2022, lakini baadae Uongozi wa Klabu hiyo ulimshtaki TFF kwa kushinikiza arejee kambini kujiunga na wenzake lakini haikuwa hivyo.

Je, una maoni gani kuhusu sakata la fei Toto na Yanga.

SOMA NA HII  YANGA YATUMIA MUDA KUWASOMA WAPINZANI WAO, KAZI INAENDELEA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here