Home Michezo YANGA SC YAISHANGAZA CAF…YAPANDA VIWANGO KWA NAFASI 48…YAACHA WATU MIDOMO WAZI

YANGA SC YAISHANGAZA CAF…YAPANDA VIWANGO KWA NAFASI 48…YAACHA WATU MIDOMO WAZI

Habari za Yanga

Habari njema kwa mashabiki wa Yanga ni timu hiyo kupanda nafasi za ubora kwa timu za Afrika mara baada ya kutinga robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Yanga hapo awali ilikuwa nafasi mbaya zaidi kwa ubora Afrika kutokana na kushindwa kufanya vyema kwa misimu mitano mfululizo katika michuano hiyo.

Yanga mara ya mwisho kutinga katika hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho ilikuwa mwaka 2018 ambapo ilimaliza wa mwisho katika kundi ambalo lilikuwa na timu za MC Algers, Rayon Sports na Gor Mahia ya Kenya.

Kitendo cha kutinga hatua ya robo fainali tena kwa kuwafunga
Monastir kwa mabao 2-0 kimewapa nafasi ya kusonga mbele kwenye viwango vya soka Afrika.

Taarifa ambazo tumezipata juu ya Yanga kupanda nafasi za ubora ni kutokana na pointi ambazo timu hiyo imezivuna mara baada ya kufuzu kwenda katika hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho.

Kabla ya kuanza kwa msimu huu wa kimataifa Yanga walikuwa wanakamata nafasi ya 75 kwa viwango vya klabu zinazoshiriki ligi ya Afrika lakini mara baada ya kufuzu na kuingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika, Yanga ilipanda mpaka nafasi ya 48.

Haikuishia hapo, juzi baada ya kushinda na kufanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho, Yanga wamepanda mpaka kufikia nafasi ya 27 hii ikiwa ni ‘performance‘ bora ya Yanga kwa msimu huu hasa kutokana na uwekezaji mkubwa uliofanywa na klabu hiyo.

Yanga imekusanya alama 10 katika michuano ya Shirikisho msimu huu. Kwa maana hiyo Yanga imepanda kwa nafasi 48 jambo ambalo limetajwa na majarida makubwa Afrika kuwa Yanga ni miongoni mwa timu ambazo zimepanda kwa kiasi kukubwa kwa viwango Afrika.

Wananchi wana nafasi zaidi ya kupanda kama watafanikiwa kuvuka hatua ya robo fainali kwenda nusu fainali, kuingia fainali na hata kutwaa ubingwa.

Aidha Tanzania imepanda mpaka nafasi ya saba katika viwango vya ubora baada ya klabu za Simba na Yanga kutinga robo fainali ya michuano ya CAF.

SOMA NA HII  ZA NDAAANII KABISA.....BAADA YA KUPIGWA 5G....USAJILI MPYA SIMBA HUU HAPA....