Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI NA WANIGERIA….EDO KUMWEMBE AIPASUKIA UKWELI YANGA…ATAJA YA TAIFA STARS…

KUELEKEA MECHI NA WANIGERIA….EDO KUMWEMBE AIPASUKIA UKWELI YANGA…ATAJA YA TAIFA STARS…

Habari za Yanga SC

Wakati Yanga SC wakijipongeza kwa ushindi wa ugenini mchezo wa mkondo wa kwanza wa Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Rivers United ya Nigeria.

Kuna baadhi ya Mashabiki wanaamini kuwa tayari Yanga SC kashamaliza mchezo kwani mchezo wa marudiano utakaopigwa Jumapili vile vile wataahinda .

Sasa mkongwe na mchambuzi wa Soka kutoka Wasafi Fm, Edo kumwembe amewatahadharisha Yanga SC kuelekea mchezo huo wa Marudiano.

Akizungumza Edo ametoa mfano wa Taifa Stars walioshinda ugenini wakachemsha nyumbani. Katika hili Edi anasema;

Majuzi Taifa Stars walitupa onyo kwamba tuendelee kuuheshimu mchezo wa soka. Walikwenda Misri wakashinda dhidi ya Uganda. Pambano la marudiano ambalo lilikuwa na hamasa kubwa kwetu tukachapwa kwa Mkapa mbele ya Waziri Mkuu. Lile ni onyo kwa Yanga wajipange.”

SOMA NA HII  SENZO ACHIMBA MKWARA MZITO, FURAHA KURUDI YANGA