Home Habari za michezo BALEKE AANDIKA REKODI HII MOROCCO…LIGI YA MABINGWA AFRIKA

BALEKE AANDIKA REKODI HII MOROCCO…LIGI YA MABINGWA AFRIKA

BALEKE APATA DENI KUBWA SIMBA...AWAOMBA MASHABIKI KUVUMILIA

Mshambuliaji wa Simba, Jean Baleke raia wa DR Congo, ameacha
rekodi matata katika ardhi ya Morocco baada ya Jumamosi iliyopita kufunga bao moja wakati timu yake ikipoteza kwa mabao 3-1 dhidi ya wenyeji wao, Raja Casablanca.

Baleke mwenye mabao matatu katika Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu, alifunga bao hilo dakika ya 48 akimalizia pasi ya Mzamiru Yassin.

Kabla ya mchezo huo, Raja Casablanca ilikuwa imecheza mechi nne za Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu kwenye Uwanja wa Mohammed V uliopo katika Jiji la Casablanca nchini Morocco bila ya kuruhusu bao.

Kitendo cha Baleke kufunga bao hilo, kimetibua rekodi ya Waarabu hao ambao wamefanikiwa kushinda mechi zote nne walizocheza hapo nyumbani kwao.

Ikumbukwe kuwa, Raja Casablanca ambao wamemaliza vinara wa Kundi C, walianzia raundi ya pili katika michuano hiyo, wakiifunga ASN Nigelec ya Niger bao 1-0, uwanjani hapo. Mechi ikichezwa Oktoba 15, 2022.

Mchezo wa pili kucheza hapo, ilikuwa hatua ya makundi dhidi ya Vipers ya Uganda uliochezwa Februari 10, 2023, wakashinda 5-0.

Februari 25, 2023 wakaichapa Horoya AC ya Guinea mabao 2-0, kabla ya Jumamosi kuichapa Simba mabao 3-1.

Kwenye Uwanja wa Mohammed V, Raja Casablanca ikiwa imecheza mechi nne za Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu kuanzia hatua ya pili, imefunga mabao 11 na kuruhusu moja pekee lililofungwa na Baleke.

SOMA NA HII  SHIKILIA HII....KILA BAADA YA DAKIKA TANO....CHOTA PESA KUPITIA CASINO HII YA MERIDIANBET...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here