Home yanga MASHINE HII HATARI YA YANGA YAREJEA…NI BAADA YA KUPATA JERAHA LA AJABU

MASHINE HII HATARI YA YANGA YAREJEA…NI BAADA YA KUPATA JERAHA LA AJABU

MASHINE HII HATARI YA YANGA YAREJEA...N BALAA AANZA MAZOEZI RASMI

KIPA wa Yanga Aboutwalib Mshery ameanza taratibu mazoezi ya viungo na ‘gym’ baada ya kufanyiwa Opresheni ya goti lake aliloumia mwishoni mwa mwaka huu akiitumikia timu hiyo.

Mshery baada ya kuumia alipata uchunguzi wa kitabibu nchini na kupatiwa matibabu lakini baada ya hapo ilionekana tatizo ni kubwa na kulazimika kupelekwa nchini Tunisia kwa oparesheni iliyofanyika mwanzoni mwa mwezi wa Februari mwaka huu na sasa anaimarika mdogo mdogo.

Akizungumza na SOKA LA BONGO, Mshery alisema anaimarika kila siku na sasa ametupa hatumii magongo tena kwenye kutembea pia ameanza mazoezi kidogo kidogo ya viungo chini ya wataalamu wa Yanga.

“Nashukuru naendelea vizuri, sasa ninafanya mazoezi madogo madogo ya kitibabu ili niendelee kuwa fiti chini ya wataalamu na muda si mrefu naamini nitaanza kufanya mazoezi ya kukimbia na mengine,” alisema Mshery aliyesajiliwa Yanga akitokea Mtibwa Sugar katikati ya msimu uliopita.

Licha ya kuimarika taratibu kwa afya ya Mshery, bado hataonekan kwenye mechi za msimu huu kwani ni muda anaotakiwa kuwa akijiweka sawa zaidi na wakati huo Yanga itakuwa ikiwatumia makipa Djigui Diarra, Erick Johora na Metacha Mnata aliyesajiliwa kwa Mkopo kutoka Singida Big Stars baada ya Mshery kuumia.

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI YA KESHO DHIDI YA WANIGERIA...MASAU BWIRE 'AWAPAKA' YANGA..AWATAJA VIONGOZI