Home Habari za michezo NEYMAR KUTIMKIA MANCHESTER UNITED…MABOSI WAKAA MEZANI…ISHU NZIMA IKO HVI

NEYMAR KUTIMKIA MANCHESTER UNITED…MABOSI WAKAA MEZANI…ISHU NZIMA IKO HVI

NEYMAR KUTIMKIA MANCHESTER UNITED...MABOSI WAKAA MEZANI...ISHU NZIMA IKO HVI

Manchester United watachukua hatua kwa ajili ya mshambuliaji wa Paris-St Germain na Brazil Neymar, 31, iwapo dau la Qatari bid, linaloongozwa na Sheikh Jassim, kwa ajili ya blabu litafanikiwa. (Sun)

Kiungo wa kati wa Borussia Dortmund na England, Bellingham, 19, ameamua kujiunga na Real Madrid lakini mataba wake bado haujaisha na klabu hiyo ya Uhispania ambayo iko tayari kumlipa Euro milioni 120. (AS – in Spanish)

Tottenham wanatarajia kupokea dau kutoka kwa Chelsea kwa ajili ya mshambuliaji wa England Harry Kane, 29, huku azma yao ya kumteua Mauricio Pochettino kama meneja ikiendelea kuongezeka (Talksport)

Mwenyekiti wa Spurs Daniel Levy ameshindwa kushawishika kwamba hatamuuza Kane to Manchester United au Chelsea, huku Mashetani Wekundu wakiwa na mshambuliaji wa Napoli na Nigeria Victor Osimhen, 24, na mshambuliaji wa Juventus na Serbia Dusan Vlahovic, 23, kwenye orodha ya wawachezaji mbadala wa Kane. (Daily Mail)

Mshambuliaji wa zamani wa Tottenham, Real Madrid na Wales Gareth Bale, 33, amekataa ombi kutoka kwa wamiliki wa klabu ya Hollywoon Wrexham Ryan Reynolds na Rob McElhenney ya kujiunga na klabu mpya iliyopanda daraja katika kurejea kwao katika Ligi ya Soka . (Sky Sports)

Brighton wanajianda kuchukua hatua kumuhusu mchezaji wa Liverpool,James Milner, 37, huku mkataba wa kiungo huyo wa kati wa England ukimalizika msimu huu. (The Athletic – subscription required)

Chelsea wanatafakari kuhusu mkataba wa mabadilishono ya wachezaji kwa ajili ya kumpata mlindalango wa Inter Milan na Andre Onana, 27, lakini Waitalia hawana nia na mlindalango Muhispania Kepa Arrizabalaga, 28. Hatahivyo wanamtamani mlinzi wa England Trevoh Chalobah, 23, na kiungo wa kati Ruben Loftus-Cheek, 27. (Gazzetta – in Italian)

Chelsea wangependelea kumuuza kiungo wa kati wa Croatia Mateo Kovacic, 28, kwa klabu iliyo nje ya Primia Ligi huku meneja wa zamani wa Blues boss Thomas Tuchel akiwa na nia ya kujiunga tena na Bayern Munich. (Evening Standard)

Mshambuliaji wa Paris St-Germain Kylian Mbappe anajaribu kumshawishi mshambuliaji wa klabu ya Eintracht Frankfurt na mchezaji mwenzake katika timu ya Ufaransa Randal Kolo Muani, 24, ajiunge na PSG msimu huu. (Christian Falk)

Arsenal wanaangalia uwezekano wa kuchukua hatua ya kuhamisho kwa ajili ya kiungo wa kati wa Chelsea na Ufaransa N’Golo Kante, 32, huku Gunners wakijua kuwa mahasimu wao wa London wanahitaji kupunguza ukubwa wa kikosi chao. (Mirror)

Mshambuliaji Mcanada Jonathan David, 23, anatarajiwa kuondoka katika klabu ya Ufaransa ya Lille msimu huu, ambayo imezifahamisha klabu kadhaa mkiwemo Tottenham, Chelsea na Paris St-Germain. (L’Equipe)

Arsenal wanaweza kuchukua hatua ya kusaini mkataba na mshambuliaji MbelgijiLois Openda, 23, kutoka klabu ya Ufaransa ya Lens msimu huu, ingawa Aston Villa pia wako makini . (Daily Mail)

Everton wanapanga kumnunua mshambuliaji wa Stoke City Tyrese Campbell, 23, msimu huu ingawa hawajui kama watanusurika katika Primia Ligi . (Football Insider)

Newcastle na Crystal Palace wanatarajia kushindwa kusaini mkataba na kiungo wa kati wa Rangers na Uskochi Calum Adamson huku mchezaji huyu mwenye umri wa miaka 15 akisaini mkataba wa kwanza wa kulipwa katika klabu ya Glasgow club. (Daily Record via Mirror)

Arsenal, Newcastle na Aston Villa zote kwa pamoja zinamuwinda kiungo wa safu ya kulia wa Real Valladolid Ivan Fresneda, 18. (90min.com)

SOMA NA HII  MCHAMBUZI:- TUSIJIDANGANYE...TAIFA STARS NI WAKAIDA MNOO MBELE YA ALGERIA....