Home Habari za Usajili Yanga YANGA YAKAMILISHA USAJILI HUU…”HII NI ZAWADI KWA MASHABIIKI WETU

YANGA YAKAMILISHA USAJILI HUU…”HII NI ZAWADI KWA MASHABIIKI WETU

YANGA YAKAMILISHA USAJILI HUU...

Tuliahidi na tumetimiza Na hii ndio zawadi ya Iftar kwa Wananchi! Hii ni kauli ya Klabu ya Yanga baada ya kutangaza kumuongezea
mkataba beki wao, Dickson Job.

Job amesaini mkataba mpya wa miaka miwili wa kuendelea kuitumikia Yanga SC.

Job mwenye uwezo wa kucheza kama beki wa kati na beki wa kulia amesaini mkataba huo mbele ya Rais wa Klabu ya Yanga Eng Hersi Said utakaomuweka Klabuni mpaka 2025.

Kitasa huyu alijiunga na Yanga, Januari kwenye dirisha dogo la msimu 2020/21 akitokea Mtibwa Sugar, amekuwa nguzo muhimu kwa Yanga katika nafasi ya ulinzi.

Kwenye misimu miwili aliyokuwa na Yanga, Job amefanikiwa kushinda mataji manne [ Ligi Kuu, Kombe la Shirikisho la Azam na mataji mawili ya Ngao ya Jamii.

Job pia ameingia kwenye rekodi ya kikosi cha Yanga kilichocheza mechi 49 za Ligi Kuu bila kupoteza, na kuwa timu ya kwanza Tanzania kuwa na idadi hiyo ya michezo na ya nne kwa Afrika.

Akizungumza na SOKA LA BONGO baada ya kusaini mkataba huu, Job alikiri kuwa kulikuwa na ofa nyingi mezani lakini moyo wake bado ulihitaji kuendelea kuitumikia Yanga SC.

“Nimefurahi sana kuongeza mkataba. Yanga ni Klabu kubwa ambayo kila mchezaji angetamani kuichezea. Nimeongeza miaka mingine miwili hapa na niwaahidi mashabiki kuwa nitaendelea kujituma zaidi.

“Ni kweli kulikuwa na ofa nyingi lakini moyo wangu uliniambia nibaki hapa ili niendelee kuwatumikia wananchi. Naamini nitafanikiwa zaidi hapa kwa miaka miwili ijayo,” alisema Job ambaye ni nahodha msaidizi wa Yanga.

SOMA NA HII  ROBERTINHO AFUNGUKA KUHUSU SIMBA ALIYEITENGENEZA ISHU IKO HIVI KWENYE MATAJI