Home Habari za michezo A-Z JINSI YANGA SC WALIVYOWEKA REKODI YA HESHIMA JANA…DONDOO MUHIMU HIZI HAPA..

A-Z JINSI YANGA SC WALIVYOWEKA REKODI YA HESHIMA JANA…DONDOO MUHIMU HIZI HAPA..

Habari za Yanga SC

WANANCHI wanacheka tu kwa kile ambacho kimetokea kwa chama lao la Yanga SC kuweka historia ya kutinga kwa mara ya kwanza hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Yanga SC imetinga hatua hiyo baada ya kuifunga Rivers United kwa jumla ya mabao 2-0 ambayo waliyapa kwenye mchezo wa kwanza nchini Nigeria kabla ya kutoka suluhu kwa Mkapa.

Vijana hao wa Nasreddine Nabi watacheza dhidi ya Marumo Gallants F.C. ya Afrika Kusini kwenye hatua ya nusu fainali.

Marumo ambayo iliitoa Pyramid ya Misri ni timu ambayo inashika nafasi ya tatu kutoka mkiani kwenye msimamo wa Ligi ya Afrika Kusini.

Hizi ni dondoo muhimu za mchezo wa robo fainali ya pili kwa Yanga ambapo wametoka suluhu dhidi ya Rivers na kutinga hatua hiyo.

Kwa mara ya kwanza msimu huu, Nabi aliamua kuanza na washambuliaji Fiston Mayele na Clement Mzize kwa pamoja kwenye safi ya ushambuliani ya kikosi hicho.

Ndani ya dakika 90 za mchezo huo, Yanga ilipiga mashuti 12 huku mawili kati ya hayo yakilenga lango, Rivers ilipiga manne na hakuna ambalo lililenga lango.

Ni kadi mbili tu ambazo zilionyeshwa kwenye mchezo huo, zote ni za njano, moja ilikuwa kwa Khalid Aucho kwa Yanga na nyingine kwa Ohaegbu.

Yanga iliotea mara moja tu huku Rivers ikiotea mara tatu huku zikishuhudiwa kona tano zikichongwa tatu kwa Yanga na mbili kwa timu hiyo ya Nigeria.

Mayele na Azizi Ki ndio wachezaji ambao walipiga mashuti mengi zaidi (3) kwenye mchezo huo wa robo fainali ya pili.

Huu ulikuwa mchezo wa nne kwa Yanga kucheza kwenye michuano ya Kimataifa huku akishindwa kupata bao tangu kwenye hatua za awali.

SOMA NA HII  KIBEGI CHA SIMBA SC KIMESHAFIKA KILIMANJARO, UZI HUU HAPA