Home Habari za michezo BAADA YA ‘KUFA KIUME’ MOROCCO…MBRAZAILI SIMBA AANZA USAJILI FASTA….MASTAA HAWA KUTUA MSIMBAZI….

BAADA YA ‘KUFA KIUME’ MOROCCO…MBRAZAILI SIMBA AANZA USAJILI FASTA….MASTAA HAWA KUTUA MSIMBAZI….

Habari za Simba SC

SIMBA SC imekubali kutupwa nje ya Ligi ya Mabingwa Afrika ikiishia robo fainali, lakini kocha Robert Olivieira ‘Robertinho’ ameibuka na gia kubwa akiwataka mabosi haraka kuanza mchakato wa kusajili mastaa wawili.

Taaarifa za uhakika kutoka ndani ya Simba SC mabosi wa timu hiyo wameingia msituni kuanza mchakato kusaka mshambuliaji wa kati mwenye makali ambaye atawapa heshima kubwa akiungana na Mkongomani Jean Baleke endapo atasalia.

Baleke yupo Simba SC kwa mkopo akitokea TP Mazembe ya DR Congo ingawa Simba na hata mchezaji mwenyewe anataka kubaki klabuni hapo kwa muda mrefu zaidi, lakini uamuzi wa mwisho utabaki kwa Mazembe ikiwa itakubali kumbakisha.

Robertinho amewaambia mabosi wake kwamba mchakato huo uanze haraka ili kuwawahi mastaa ambao wamefanya vizuri msimu huu eneo la ushambuliaji kabla ya msimu huu kumalizika kwa kuwa watapanda bei.

“Kocha ametuambia tuanze haraka kutafuta mshambuliaji wa kati hilo ni hitaji lake la kwanza kwa msimu ujao, tunakubaliana naye ingawa tuna Baleke (Jean) lakini bado kuna haja ya kupata mtu bora zaidi,”alisema bosi mmoja wa juu wa Simba.

“Kwanza hatuna uhakika kama Baleke atabaki kwetu zaidi. Kwa hiyo hiyo kazi tumeshaanza kukimbizana nayo, lakini hata yeye pia anatafuta akipata atatuambia kisha tutapima na sisi tulichokipata kisha tutafanya uamuzi.

”Mbali ya mshambuliaji wa kati, hitaji lingine la Robertinho ni kuletewa beki katili wa kati atakayekuja kuungana na Mkongomani mwingine, Henock Inonga.Hesabu hizo ni wazi Simba hairidhiki na mwendelezo wa huduma ya beki Joash Onyango ambaye ameonekana kuendelea kutokuwa na kiwango bora kwenye eneo la ulinzi.

Simba pia itaachana na beki raia wa Ivory Coast, Mohamed Outtara ambaye ameendelea kulizoea benchi kuliko kucheza katika kikosi cha kwanza.Robertinho amekubaliana na kiwango cha Inonga na kazi ya maana anayoendelea kuipiga, lakini amemkata maini Onyango akiona ni mtu ambaye Simba haipaswi kumtegemea katika malengo ya msimu ujao.

“Ukiacha mshambuliaji pia tuna kazi nyingine ametutaka kutafuta beki wa kati pia mwenye ubora kama Inonga, haoni (Robertinho) kama ataendelea na Onyango lakini hata yule Outtara naye tutaangalia namna ya kuachana nao mwisho wa msimu.”

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI YA CAF KESHO....UNAAMBIWA NABI HUKO YANGA HATAKI MZAHA...APANIA KUUA 'SISIMIZI KWA RUNGU'....