Home Habari za michezo BAADA YA KUTINGA FAINAL CAF…YANGA WAKATAA ‘VIBE’ LA MASHABIKI DAR….ISHU IKO HIVI…

BAADA YA KUTINGA FAINAL CAF…YANGA WAKATAA ‘VIBE’ LA MASHABIKI DAR….ISHU IKO HIVI…

Habari za Yanga

Wakati Kikosi cha Yanga kikiandika Historia ya kutinga Fainali ya Kombe la Shirikisho kwa mara ya kwanza katika historia yake.

Wakati Yanga wakitengeneza Historia hiyo, wapo katika ardhi ya ugenini Afrika ya Kusini wakiichapa Marumo Gallants mabao 2-1 na kushinda ushindi wa jumla 4-1.

Kutokana na rekodi hiyo bila shaka Mashabiki wa Yanga wanaisubiri kwa hamu Timu yao kwa ushujaa huo lakini hali ni tofauti kwa uongozi wa Yanga.

Kupitia Afisa Habari wa Klabu ya Yanga, ameandika ujumbe akiwaasa Mwapenzi na Mashabiki kutijitokeza kuipokea Timu hiyo.

Ali kamwe ameandika;

“Najua Furaha ni kubwa sana, Lakini Uongozi wa Yanga unawaomba mashabiki wetu kuendelea kuiombea Dua na kuisapoti Timu yetu kwenye mechi muhimu zinazofata

1: Nusu Fainali ya ASFC 2: Fainali ya CAF

Hivyo tunaomba kusiwe na Mapokezi yoyote AIRPORT kwa sasa..”

SOMA NA HII  MRUNDI WA YANGA APEWA PROGRAM MAALUMU