Home Habari za michezo SIMBA TENAAH!!!…WAPOTEZA TENA UBINGWA LIGI YA WANAWAKE…MABINGWA WAPYA HAWA HAPA..

SIMBA TENAAH!!!…WAPOTEZA TENA UBINGWA LIGI YA WANAWAKE…MABINGWA WAPYA HAWA HAPA..

Habari za michezo

Timu ya JKT Queens imefanikitwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara baada ya ushindi wa Mabao 7-2 dhidi ya Mkwawa Queens jana Uwanja wa Samora mjini Iringa.

Wapinzani wao wakuu katika mbio za ubingwa na waliokuwa mabingwa pia, Simba Queens ambao leo wameshinda bao 1-0 dhidi Ceasiaa Queens Uwanja wa Chuo Kikuu cha Mkwawa mjini Iringa pia.

Kwa matokeo hayo, JKT Queens inamaliza na pointi 46, moja zaidi ya Simba Queens, wakati Fountain Gate Princess iliyomaliza na pointi 41 imeshika nafasi ya tatu na Yanga Princess yenye pointi 34 ni ya nne.

JKT Queens wanatwaa ubingwa bila kupoteza mechi yoyote (Unbeaten). Wamefikia rekodi ya Simba ya kuchukua kombe mara 3 ambapo wamebeba msimu wa 2017/18, 2018/19 na 2022/23

SOMA NA HII  KUHUSU NANI ATAKUWA BINGWA MSIMU HUU...EDO KUMWEMBE AIBUKA NA HILI...AITAJA YANGA KWA SABABU HIZI...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here