Home Habari za michezo JAMBO JIPYA LA YANGA HILI HAPA…SIMBA HAWAJAWAHI KUFIKIA REKODI HII KAMWE…

JAMBO JIPYA LA YANGA HILI HAPA…SIMBA HAWAJAWAHI KUFIKIA REKODI HII KAMWE…

Habari za Yanga

NI msimu wa kicheko kwa Yanga baada ya muendelezo wa kufanya vizuri kwenye mashindano mbalimbali, ikiwemo mechi yao na Singida Big Stars |(SBS) mechi ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC), iliyopigwa Uwanja Liti mkoani Singida.

Ushindi wa Yanga wa bao 1-0 dhidi ya SBS umeifanya itinge hatua ya ASFC ambapo itakutana na Azam FC iliyoitoa Simba hatua ya nusu fainali kwenye kinyang’anyiro hicho.

Yanga ilipata bao dakika 82 kupitia kwa Fiston Mayele ambaye aliingia dakika ya 77, Kennedy Musonda alipiga ukaokolewa na kumkuta beki wa Singida ambapo Nkane akapiga shuti lake kipa Benedict Haule kautema ndipo Mayele kauunga.

Ushindi ambao unaendeleza raha ya mashabiki wao baada ya kufanya vizuri kwenye michuano tofauti.

Yanga imenyakua ubingwa wa Ligi Kuu Bara mara mbili mfululizo, imetinga fainali za Kombe la Shirikisho Afrika na ilichukua taji la Ngao ya Jamii.

MCHEZO ULIVYOKUWA
Kama dakika sita ambazo ni sawa na dakika ya 51, SBS ilicheza kwa Kasi ambapo Gomes Bruno alimpa pasi Francis Kazady aliyepiga shuti Kali lakini kipa wa Yanga,Metacha Mnata alikuwa makini kupangua.

Dakika 10 za kipindi cha pili wachezaji wa timu hizo walikuwa wanatumia sana nguvu , huku wakiwa wanafika miguuni kiasi kwamba rafu zilichukua nafasi, baada ya dakika hizo ambazo sawa na dakika 55 i mpira ulipooza.

Dakika 77 bila goli zilimfanya kocha Nabi kufanya mabadiliko ya wachezaji watatu waliyoingia ni Mayele, Kennedy Musonda na Tuisila Kisinda, wakitoka Mziza, Aziz Ki na Jesus Moloko, baada ya hapo Yanga ilibadilika kimchezo ilianza kwa Kasi na dakika ya 82 Mayele alifunga bao.

Bao hilo la Mayele Musonda alipiga v, ambayo ilimkuta Nkane aliyepika shuti kipa Haule akautema ndipo staa huyo kutoka Congo akaunga mpira nyavuni, ambapo Sabu hizo na Nabi zilimzalia matunda na kuleta furaha kwa mashabiki.

DAKIKA 45 ZA KWANZA
Kipa wa Singida Big Stars, Benedict Haule alikumbana na mashuti ya wachezaji wa Yanga,uimara wake wa kuzisoma hatari zikiwa mbali ulifanya timu yake kumaliza salama dakika hizo.

Pamoja na Yanga kufika mara kwa mara golini kwa SBS, ilikumbana na wakati mgumu kutoka kwa mabeki wakiongozwa na mzoefu Pascal Wawa hakuwa na kasi ila utulivu ulimfanya atumie akili kumsaidia kipa Haule baadhi ya hatari alizizuia kutofika golini.

Viungo wa SBS walijitahidi kucheza vyema kati, ambapo mashambulizi yao yalikuwa yakushitukiza akionekana Gomes Brouno kufika golini na pasi alizokuwa anatengenezewa na Deus Kaseke aliyecheza kwa kiwango cha juu,kilichokuwa kinawapa presha baadhi ya mashabiki wa Yanga waliokuwa wamekaa VIP.

Laiti kama mashuti ya mbali aliyekuwa anayapiga Aziz Ki akitokea pembeni si chini ya matatu yangelenga bao basi Yanga ingweza kutoka kipindi cha kwanza kwa mabao zaidi ya matatu.

Hiyo ilikuwa ni nusu fainali ya saba kwa Yanga kati ya misimu nane mfululizo wa michuano hiyo ikiwa ni rekodi ya aina yake kwa wababe hao wa soka la Tanzania.

Ni msimu mmoja tu wa 2017-2018 ndio Yanga ilishindwa kuingia nusu fainali baada ya kutolewa mapema, lakini misimu mingine iliyosalia tangu michuano hiyo iliporejeshwa tena mwaka 2015 baada ya kusimama kwa muda mrefu wakati ilipokuwa ikifahamika kama michuano ya Kombe la FA 2002 ilitinga nusu fainali mara saba.

SOMA NA HII  YANGA WATOA TAMKO BAADA YA KUPOTEZA MBELE YA WANAIJERIA KWA MKAPA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here