Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI YA FAINAL CAF…NABI ATAMBA KUPATA MKANDA MZIMA WA WAARABU MAPEMA..

KUELEKEA MECHI YA FAINAL CAF…NABI ATAMBA KUPATA MKANDA MZIMA WA WAARABU MAPEMA..

Habari za Yanga SC

KOCHA mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi amefanikiwa kunasa faili ya USM Alger kwa kubaini ubora na madhaifu ya mpinzani wao huyo kuelekea mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Mchezo wa fainali Yanga wataanzia nyumbani utakaopigwa Mei 28 katika uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam na marudiano ni Juni 3, mwaka huu nchini Algeria.

Nabi alisema tayari viongozi wameshatafuta baadhi ya video za mechi walizocheza hivi karibu USM Alger na kufanyia kazi kabla ya kukutana na wapinzani wao hao.

Alisema baada ya kupata uhakika wa kucheza fainali aliwataka viongozi kupata baadhi ya michezo ya wapinzani wao kuwafatilia jinsi wanavyocheza na kufanika kazi mbinu za kiufundi.

β€œMechi itakuwa ya ushindani mkubwa nahitaji kuwafatilia wapinzani wetu jinsi wanavyocheza wanapokuwa ugenini na nyumbani, Hii ni fainali itakuwa mechi ya ushindani mkubwa, tunatakiwa kuwafahamu wapinzani wetu vizuri,” alisema Nabi.

Alisema kuangalia wachezaji wao bora ambao hawataleta madhara katika mchezo huo wataanza kucheza mchezo wa kwanza ambao watacheza nyumbani.

Nabi aliongeza kuwa wanakuwa makini kuwasoma na kuona ubora wa wapinzani wao watakaokutana nao katika fainali.

“Niwapongeze wachezaji wangu wamepambana na kufanikiwa kusonga mbele bado kama benchi la ufundi tuna kazi ya kufanya kuelekea fainali ili tutwaa ubingwa wa Afrika,” alisema Nabi.

Alisema pia anashukuru viongozi wa Yanga kwa kushirikiana naye bega kwa bega kuanzia mwanzo mwa msimu kufanya usajili mzuri na kuhakikisha wanapata mahitaji yote.

Kocha huyo alisema tayari ameanza kuwafatilia wapinzani wake wanapokuwa ugenini au nyumbani kuona jinsi wanavyocheza na kubaini mbinu zao.

Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa Yanga kutinga fainal ya mashindano ya CAF, huku ikiwa ni mara ya pili kwa timu kutoka Tanzania kufanya hivyo ambapo Simba walifanya hivyo kwa mara ya kwanza mwaka 1993.

Kwa mujibu wa viwango vya ubora wa CAF, Klabu ya Yanga iko katika nafasi ya 22, ambapo kama itatawa ubingwa huo itapanda mpaka nafasi ya 15 huku ikiifanya Tanzania kuwa na alama 35 na kuipandisha mpaka nafasi ya 5 kwa ubora kwenye upande wa Ligi.

Hata hivyo, Yanga wananafasi kubwa ya kujihakikishia pia kitita kikubwa cha pesa kama sehemu ya zawadi kwa mshindi wa kombe la Shirikisho, ambapo bingwa wake hupata zaidi ya Bilioni 2 za kitanzania.

Mbali na hivyo, Yanga pia itakuwa na uhakika wa moja kwa moja bila kujali nafasi yake kwenye ligi ya nchi, kucheza michuano ya Ligi ya Mabingwa msimu ujao ambapo wataanzia hatua ya kwanza.

Hii itaenda sambamba na kuifanya Yanga kupata nafasi ya kushiri mashinado mapya ya CAF Super League ambapo safari hii kwa ukanda wa CECAFA ni Simba tu wanaowakilisha .

SOMA NA HII  REREKODI ZAIBEBA YANGA MBELE YA SIMBA