Home Habari za michezo FT YANGA 1-2USMA…MAYELE APIGA GOLI LA KIDEO…SHABIKI AFARIKI, 40 MAJERUHI….SERIKALI YATOA TAMKO…

FT YANGA 1-2USMA…MAYELE APIGA GOLI LA KIDEO…SHABIKI AFARIKI, 40 MAJERUHI….SERIKALI YATOA TAMKO…

Yanga vs USMA

YANGA SC imejiweka katika mazingira magumu ya kutwaa Kombe la Shirikisho barani Afrika baada ya kufungwa mabao 2-1 na USM Alger mchezo wa kwanza wa Fainali ya Michuano hiyo uliochezwa dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

USM walipata bao la ushindi dakika ya 32 likifungwa na Aimen Mahious bao lililowapeleka wageni mapumziko wakiwa mbele ya bao hilo.

Mshambuliaji hatari kwa Sasa ndani na nje Fiston Mayele alifunga bao dakika ya 82 likiwa bao lake bao lake la saba katika michuano hiyo dakika ya 84 wageni walipata bao la pili likifungwa na Khaled Bousseliou dakika mbili tu baada ya bao la Mayele.

Kwa matokeo hayo Yanga wanatakuwa kwenda kupata ushindi wa kuanzia mabao mawili na kuendelea ili waweze kutwa ubingwa wa michuano hiyo mchezo wa marudiano utapigwa Juni 3,mwaka huu nchini Algeria.

Yanga vs USMASHABIKI AFARIKI, 40 WAJERUHIWA.

Aidha katika hatua nyingine, Leo katika Uwanja wa Benjamini Mkapa Yanga ikicheza fainali Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USM Alger, wakati msongamano wa mashabiki wakiingia uwanjanni muda mchache kabla ya mechi umesababaisha kifo cha mtu mmoja na wengine wajeruhiwa.

Taarifa hiyo imetolewa na Waziri wa afya Ummy Mwalimu kupitia akaunti yake mtandao wa Twitter ametoa taarifa ya hali iliyotokea Uwanja wa Mkapa baada ya mashabiki kusongamana nje ya mageti na mengine kuvunjwa na mashabiki kuingia kwa nguvu uwanjani na hadi sasa majeruhi ni 30 huku mtu mmoja anayekadiriwa kuwa na miaka 40 amefariki dunia.

“Timu ya wataalam wa Huduma za Dharura ya Hospitali ya Taifa Muhimbili imeshawasiliana na Hospitali ya Rufaa Ya Mkoa Temeke na wapo standby kupokea na kuwahudumia majeruhi ambao watahitaji matibabu zaidi,” ameeleza Waziri Ummy

Msongamano wa mashabiki kuingia uwanjani ulikuwa mkubwa na kila ambapo watu wa usalama walipokuwa wakiwazuia geti moja walikimbilia lingine na kuingia.

SOMA NA HII  BENCHIKHA ALIVYOIBADILISHA SIMBA KUWA YA MOTO ZAIDI...ROBERTINHO ALIFELI HAPA...