Home Habari za michezo HUYU NDIO ‘PROF’ NABI SASA….UNAAMBIWA BAADA YA KUWATUPA WANIGERIA..FASTA KAENDA SAUZI…

HUYU NDIO ‘PROF’ NABI SASA….UNAAMBIWA BAADA YA KUWATUPA WANIGERIA..FASTA KAENDA SAUZI…

Habari za Yanga SC

Kocha Mkuu wa Yanga SC, Nasreddine Nabi amesema wataisoma Klabu ya Marumo Gallants na kutengeneza mpango mkakati wa kuwavaa kwenye mchezo wa nusu fainali ya kombe la shirikisho Afrika.

Nabi amesema hayo jana Aprili 30, 2023 katika Dimba la Mkapa mara baada ya kufanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa kuiondoa Rivers United ya Nigeria.

“Tutaifuatilia kwanza timu ambayo tunakwenda kukutana nayo kisha tutapanga mpango mkakati wa namna ambavyo tutacheza nayo. Kila timu ina namna yake ya kucheza na mechi hazifanani.

“Tutaisoma Gallants itakuwaje na tukiwasoma tutajua namna ya kujipanga, kisha mengine tutamwachia mungu,” amesema Nabi.

Yanga SC itakutana na Marumo Gallants katika hatua ya nusu fainali ambapo mchezo wa kwanza utapigwa katika dimba la Mkapa, Mei 10, 2023 kisha mchezo wa marudiano utapigwa nchini Afrika Kusini Mei 17, mwaka huu.

SOMA NA HII  ISHU YA MKATABA WA CHAMA WAVUJA, VIONGOZI WA SIMBA WAHAHA ISHU IKO HIVI