Home Habari za michezo KUHUSU KUBADILI MFUMO WA NGAO YA JAMII…UKWELI HUU HAPA…SIMBA NA YANGA BADO...

KUHUSU KUBADILI MFUMO WA NGAO YA JAMII…UKWELI HUU HAPA…SIMBA NA YANGA BADO ZIKO..

Habari za Michezo

Kabla ya kuanza kwa msimu huu 2022/23 kulifanyika mabadiliko ya kanuni za ligi kuu ya NBC mojawapo ya mabadiliko ni kanuni ya (19:1) kuhusu mchezo wa Ngao ya jamii ambapo kwa sasa kutakuwa na shindano la Ngao ya Jamii na sio mchezo mmoja.

Kanuni ya 19.1 inasema kutakuwa na shindano la Ngao ya jamii, ambapo timu tatu (3) za juu kwenye ligi kuu ya NBC na Bingwa wa kombe la shirikisho (ASFC) zitacheza mchuano huo maalumu. Endapo Bingwa wa FA yumo kwenye timu (3) za juu, basi ataingia anayeshika nafasi ya (4) kwenye ligi kuu.

Kwa Sasa ilivyo ni wazi Yanga, Simba, Azam na Singida ndio zitakazocheza shindano maalumu kwa kuanza kwa michezo ya nusu fainali.

Toka mfumo wa kucheza ngao ya jamii urudi rasmi, Klabu za Simba na Yanga zimekuwa zikipotezana kutwa taji hilo, huku Simba wakibeba mara nne na yanga wakishinda mara moja.

Mechi ya mwisho ilikuwa mwanzoni mwa msimu huu ambapo Bingwa wa Ligi (Yanga) alicheza na aliyeshika nafasi ya pili (Simba).

Shirikisho la Soka nchini, hutoa sehemu ya mapato ya mechi hii kwenda kwenye shughuli za kijamii, ambapo mara kadhaa jamii faidika ya pesa hizo imekuwa ni ya watu wa Dar pekee.

Mbali na hayo, mchezo huo hujawahi kupigwa nnje ya jiji la Dar es Salaam, toka kuja kwa mfumo huu mpya ambapo Simba wameonekana wakitawala zaidi.

SOMA NA HII  NANI BORA KATI YA PACOME NA CHAMA..?..KOCHA LA CAF LAMPA TUZO HUYU...