Home Habari za michezo MAYELE: AZAM WAKICHEZA NATIMU NDOGO UTASHANGAA …ILA NGOJA WACHEZE NA SIMBA AU...

MAYELE: AZAM WAKICHEZA NATIMU NDOGO UTASHANGAA …ILA NGOJA WACHEZE NA SIMBA AU YANGA…

Habari za Yanga

Mshambuliaji kinara wa Klabu ya yanga, Fiston Mayele amesema kuwa licha ya Azam FC kukamia mechi kubwa, lakini ana uhakika watapambana ili kufanikiwa kupata ubingwa wa Kombe la Shirikisho (ASFC).

Mayele amesema hayo wakati akizungumza na wanahabari mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa nusu fainali kati ya Yanga na Singida Big Stars huku akifunga bao pekee lililoipeleka Yanga fianli.

“Mchezo wa fainali utakuwa mgumu kwa sababu Azam FC wana wachezaji wazuri na benchi zuri la ufundi. Lakini hiyo haituzuii sisi kupambana na kuhakikisha tunauchukua tena ubingwa huo tuliouchukua mwaka jana.

“Tunajua Azam FC wanapenda kukamia mechi kuwa, ukitaka kuwaona wachezaji wao basi wakutane na Yanga au Simba, wanakamia kinoma, lakini wakikutana na Namungo au timu nyingine wanakuwa wa kawaida wala huwezi kuwaona, kwa hiyo tunajua utakuwa mpambano mgumu,” amesema Mayele.

Mchezo wa Fainali kati ya Yanga na Azam FC utapigwa jijini Tanga katika Uwanja wa CCM Mkwakwani watakayokutana na Azam FC.

SOMA NA HII  FT: BIASHARA UTD 1-1 YANGA ....MAYELE KAMA KAWA JAPO SIO KIVILEE...WAKIZIDI KUZINGUA SIMBA BADO YUMO UJUE...