Home Habari za michezo SIMBA WAINGILIA KATI DILI LA DILUNGA NA JKT….MAMBO YAGEUZWA ‘JUU CHINI’ HARAKAHARAKA…

SIMBA WAINGILIA KATI DILI LA DILUNGA NA JKT….MAMBO YAGEUZWA ‘JUU CHINI’ HARAKAHARAKA…

Habari za Simba

Fununu za kiungo mshambuliaji, Hassan Dilunga kuhusishwa kwenye usajili wa msimu ujao wa Ligi Kuu Bara na JKT Tanzania huenda mambo yakabadilika kwani mchezaji huyo anaweza kupewa mkataba wa mwaka mmoja na Simba.

Simba ina mpango ya kumsainisha mkataba huo mchezaji huyo, wakati huohuo JKT Tanzania ilikuwa inahitaji huduma yake lakini ni kama timu hiyo imerudi nyuma hatua moja, baada ya kuona bado hayupo fiti.

Kocha wa timu hiyo, Malale Hamsini alisema anahitaji kusajili wachezaji wenye kiwango cha juu ambao wataonyesha ushindani, kwani hawataki yajirudie mambo ya miaka ya nyuma yaliyowashusha daraja.

“Ripoti niliyowapa viongozi ni kunisajilia wachezaji nafasi tatu ambazo ni mshambuliaji, kiungo na beki ili kupata nguvu maeneo hayo ambayo yataongeza changamoto;

“Tunaingia kwenye ushindani mkubwa, tunahitaji kuwa bora kila eneo kuhusiana na Dilunga bado hatujamsainisha hilo naliacha kwa viongozi ni kweli tulikuwa naye kwenye mazoezi na nimemuona,” alisema Malale.

Malele alisema wanatambua ugumu wa ligi hawatafanya makosa kwenye usajili lengo ni kuona timu hiyo hairudii makosa na kujikuta inarudi Championship tena.

Alisema wataongeza wachezaji wachache watakaoongeza ushindani kwa waliopo ambao waliipambania timu kuanzia chini na kuipandisha kwani wana uwezo mzuri ila wanahitaji kuongezewa nguvu.

SOMA NA HII  AZAM FC WAJIBU MAPIGO KWA SIMBA NA YANGA...WASHUSHA KINDA LA TIMU YA TAIFA YA IVORY COAST..NI BALAA NA NUSU...