Home Azam FC MANULA, KAPOMBE WAIBUA JAMBO AZAM FC…MABOSI WAANZA ‘KUCHANGA KARATA UPYA”…

MANULA, KAPOMBE WAIBUA JAMBO AZAM FC…MABOSI WAANZA ‘KUCHANGA KARATA UPYA”…

Habari za Simba leo

Uongozi wa Azam FC umesema kuwa hautakubali kufanya makosa ya kuwaachia mastaa wao kuondoka bure mwishoni mwa msimu huu na badala yake haraka watafanya maboresho ya mikataba kabla ya kumalizika mwishoni mwa msimu huu kwa baadhi ya wachezaji akiwemo Prince Dube na James Akaminko.

Hiyo ni katika kuelekea dirisha kubwa la usajili kufunguliwa kwa ajili ya msimu ujao, Azam FC na Singida Big Stars watakwenda kuiwakilisha nchi katika Kombe la Shirikisho Afrika.

Simba msimu wa 2017 iliwasajili nyota wanne kwa mpigo kutoka Azam FC, kama wachezaji huru ambao ni John Bocco, Aishi Manula, Shomari Kapombe na Erasto Nyoni.

Usajili wa nyota hao ulionekana kuipa mafanikio makubwa Simba ambao walifanikiwa kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu Bara mara nne mfululizo na Kombe la FA kwa misimu miwili kutokana na ubora wa kikosi chao.

Dube ambaye ameifunga Simba mara tatu mfululizo katika msimu huu katika ligi mara mbili walipokutana nyumbani na ugenini, pia katika Nusu Fainali ya Kombe la FA.

Akizungumza nasi, Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin ‘Popat’ alisema kuwa, walifanya makosa makubwa kuwaacha wachezaji hao akina Nyoni, Bocco, Manula na Kapombe ambao walikwenda kuipa mafanikio makubwa Simba.

Popat alisema kuwa, wanafahamu walipokosea na hawatarudia tena kufanya makosa na badala yake watahakikisha wanawaongezea mikataba mipya nyota wao muhimu mikataba kabla ya kumalizika.

“Kapombe, Nyoni, Manula, Bocco tulifanya kosa kuacha mikataba yao mpaka inakaribia mwishoni, wale hatukuwauzia Simba waliondoka huru. Hatuwezi kufanya makosa tena yaliyosababisha wachezaji wanne wakaondoka msimu ujao.

“Tulichopanga kuwaboreshea mikataba wachezaji wetu ambao mikataba yao inatarajiwa kumalizika kabla ya msimu kumalizika kwa lengo la kutoa nafasi kwa baadhi ya timu za hapa nchini kuwachukua kama tulivyofanya awali.

“Lipo wazi Azam hivi sasa ina wachezaji wengi bora msimu huu na hii ni kutokana na skauti kubwa inayofanywa na viongozi kuhakikisha timu inakuwa imara na tishio katika msimu huu,” alisema Popat.

SOMA NA HII  MRWANDA AFICHUA KILICHO NYUMA YA UBOVU WA SIMBA..AWATAJA WACHEZAJI NA NAMNA WALIVYOTUMIKA....

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here