Home Habari za michezo MASHINE YA KAZI HII HAPA….MABOSI SIMBA NA YANGA WAVIZIANA AIRPORT…

MASHINE YA KAZI HII HAPA….MABOSI SIMBA NA YANGA WAVIZIANA AIRPORT…

Tetesi za Usajili Bongo

Beki wa Kati wa Kabwe Warrior ya Zambia, Marcel Kalonda raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo anahusishwa na klabu zenye misuli ya kiuchumi Tanzania [Singida Big Star, Simba, Yanga na Azam FC].

Baada ya kuonesha kiwango kikubwa kwenye Ligi ya Zambia kwa kutwaa mataji manne ya Ligi hiyo akiwa na Zesco United ikiwa ni pamoja na kucheza Robo Fainali mbili mfululizo za Ligi ya Mabingwa Afrika [2018|19 na 2019|20].

Wakati msimu unaelekea mwishoni, tayari baadhi ya klabu zimeanza mipango ya kuimarisha vikosi vyao baada ya kuona mapungufu yakiyojitokeza kipindi chote cha msimu huu.

Endapo Marcel Kalonda atafanikiwa kutua Tanzania ataungana na wachezaji wengi raia wa DR Congo wanaocheza Ligi Kuu na Ligi ya Championship.

SOMA NA HII  KABLA HATA YA GAME NA MAMELOD YANGA YAPELEKWA NUSU FAINAL ....