Home Habari za michezo CHELSEA KUMSHUSHA MANE NA POCHETTINO STAMFORD BRIDGE…

CHELSEA KUMSHUSHA MANE NA POCHETTINO STAMFORD BRIDGE…

Habari za Kimataifa

Meneja mtarajiwa wa Kikosi cha Chelsea, Mauricio Pochettino ameripotiwa kupitisha mpango wa usajili wa mshambuliaji wa FC Bayern Munich ya Ujerumani Sadio Mane ili atue kukipiga Stamford Bridge katika dirisha lijalo la usajili.

Mane mwenye umri wa miaka 31, amekuwa akikabiliwa na wakati mgumu huko Bayern tangu alipojiunga akitokea Liverpool mwaka jana na akiwa na miamba hiyo ya Bundesliga ameanzishwa kwenye mechi 17 tu za ligi msimu huu.

Hivi karibuni aliripotiwa kumpiga ngumi ya mdomo mchezaji mwenzake, Leroy Sane baada ya FC Bayern Munich kukumbana na kipigo kutoka kwa Manchester City katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, Jambo hilo linadaiwa kumtibulia sifa yake miongoni mwa mabosi wa Bayern pamoja na mashabiki wa timu hiyo na hilo linaelezwa linaweza kumsukumia Msenegali huyo kwenye mlango wa kutokea.

Kwa mujibu wa Football Insider, Mauricio Pochettino amewapa ruhusu waajiri wake wapya watarajiwa, Chelsea kwenda kukamilisha usajili wa Mane, huku kocha huyo wa zamani wa Tottenham Hotspur akidai anamkubali sana mchezaji huyo.

Bayern Munich inayonolewa na Thomas Tuchel imefungua milango ya kupokea ofa ya kuhusu winga huyo na kama kutawekwa mezani ofa ya Pauni 30 mililion basi biashara inaweza kufanyika.

Imeelezwa Mane amewekwa kwenye kipaumbele cha usajili wa dirisha lijalo la kikosi cha Chelsea, ambao wanataka kuboresha safu yao ya ushambuliaji baada ya kuonekana kuwa na shida nyingi msimu huu.

Chelsea chini ya kocha wa muda Frank Lampard usiku wa jana Jumanne ilikuwa huko Emirates kukipiga na Arsenal katika mechi ya kibabe kabisa ya Ligi Kuu England, iliyomalizika kwa kikosi chake kulele 3-1

SOMA NA HII  SINGIDA BIG STAR 'WAMCHOMOA' ONYANGO MAZIMA...