Home Habari za michezo KUHUSU DILUNGA KUPEWA MKATABA SIMBA….UKWELI WOTE HUU HAPA…

KUHUSU DILUNGA KUPEWA MKATABA SIMBA….UKWELI WOTE HUU HAPA…

Tetesi za Usajili Simba

Klabu ya Simba SC inatajwa kukamilisha usajili wa aliyekuwa kiungo wao, Hassan Dilunga baada ya kumpa mkataba wa mwaka mmoja wenye kipengele cha kuongezewa mkataba mwingine endapo atafikia kiwango kinachotarajiwa kutoka kwake.

Awali, Dilunga alikuwa anatajwa kujiunga na JKT Tanzania kutokana na ukaribu wake na bosi wa juu wa timu hiyo, lakini mabosi wa Simba SC hawakuwa tayari kumuachia kutokana na huduma yake nzuri aliyoitoa awali.

Dilunga, ambaye anamudu vyema kucheza kama kiungo mshambuliaji, alipata majeraha ya goti akiwa na Simba SC msimu uliopita na timu hiyo haikumuongezea mkataba pale ulipomalizika.

Kiungo huyo ambaye baada ya kuwa mchezaji huru aliwahi kuonekana akifanya mazoezi ya gym kwenye klabu ya Azam FC, lakini baadae alipoanza mazoezi ya uwanjani mara nyingi alikuwa akifanya na JKT Tanzania.

Katika kujiridhisha na mchezaji huyo, Simba SC ilimpa nafasi ya kufanya naye mazoezini ili kocha atakaporidhishwa na kiwango chake aweze kumsajili kwa ajili ya msimu ujao.

Mmoja wa watu wa karibu na mchezaji huyo amethibitisha kwamba Dilunga tayari ameshasaini mkataba wa mwaka mmoja na ndiyo maana ameanza mazoezi.

“Kweli alikuwa na dili la kwenda JKT Tanzania na pale ni kama nyumbani kwake kwa sababu walimlea tangu anaanza soka la ushindani, lakini mwisho wa siku waajiri wake wa zamani (Simba) wameona wamrejeshe,” kilisema chanzo hicho.

Msemaji wa Simba, Ahmed Ally alipoulizwa alisema Dilunga amerejea kwenye kikosi chao kwa sasa ili kuangaliwa na kocha na kama akifurahishwa na kiwango chake atasajiliwa.

“Ndiyo, hii ni mara yake ya pili, lakini ni muendelezo kwake kwa sababu kuna muda huwa anaacha pale tu napokuwa tuna maandalizi ya mechi kama ilivyokuwa kwa Wydad.

“Kwa sasa amerejea kwa sababu tunafanya mazoezi kwa muda mrefu ili tucheze mechi, ndiyo sehemu ambayo kocha anazidi kumuangalia kwa mara nyingine,”

Dilunga alidumu Simba SC kwa misimu minne mfululizo, akibeba taji la Ligi Kuu mara nne na Kombe la Shirikisho ‘ASFC’, kwa sasa amerejea kwa sababu tunafanya mazoezi muda mrefu kwa ajili ya kumaliza mechi za Ligi Kuu zlizobaki msimu huu.” amesema Ahmed Ally

SOMA NA HII  FT: GEITA GOLD 0-1 YANGA.....MAYELE AZIDI KUITETEMESHA LIGI KUU...MAKAMBO AISEMEA TIMU...