Home Habari za michezo WAKATI ONYANGO AKIOMBA POO …KITASA HIKI HAPA KUTUA SIMBA SC…JAMAA KAKIPIGA MPAKA...

WAKATI ONYANGO AKIOMBA POO …KITASA HIKI HAPA KUTUA SIMBA SC…JAMAA KAKIPIGA MPAKA USA…

Abdul Rwatubyaye to Simba SC

Safu ya ulinzi ya Simba inatarajiwa kuimarishwa kwenye dirisha la usajili litakalofunguliwa mwezi ujao baada ya ligi kuu 2022/23 kumalizika.

Wakati kukiwa na taarifa kuwa Joash Onyango ameomba kuachwa ili akatafute changamoto kwingine, Simba imeanza mchakato wa kumsaka mrithi wake.

Jicho la kocha Robertinho Oliveira limetua kwa Abdul Rwatubyaye mlinzi wa kati wa klab ya Rayon Sports ya Rwanda.

Rwatubyaye ambaye pia hucheza timu ya Taifa ya Rwanda, amewahi kufanya kazi na Robertinho wakati akiinoa Rayon msimu wa 2018/19.

Alirejea Rayon msimu uliopita baada ya kucheza soka la kulipwa nchini Marekani kwa misimu miwili.

SOMA NA HII  BAADA YA KUONA HAOMBI MSAMAHA WALA HANA SHIDA...SIMBA WAMCHIMBWA MKWARA WA KUFA MTU MORRISON...