Home Habari za michezo AHMED ALLY:- NI FEDHEHA KWETU KUWANGALIA YANGA WAKICHEZA…SIMBA TUNAPASWA KUAMKA..

AHMED ALLY:- NI FEDHEHA KWETU KUWANGALIA YANGA WAKICHEZA…SIMBA TUNAPASWA KUAMKA..

Habari za Simba SC

Afisa Habari wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally ametupia jiwe kwa watani wao Yanga baada ya kupoteza fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Mabingwa USM Alger kwa faida ya goli la ugenini.

“Wamejitahidi nini?? Wamekufa kiume gani?! Wamepambana kitu gani?

Yaani kufungwa na timu ambayo inashika nafasi ya 10 kwenye ligi yao ni kujitahidi

Kufungwa na timu ambayo ni ngeni ni kwenye mashidano ya Afrika ni kufa kiume

Hapo wameambulia fedheha tuu, wamecheza na timu wanayolingana nayo hakuna cha kujitahidi,” ameandika Ally.

Pia ameandika , UTO kakosa kombe tumefurahi na ukweli hatuwezi kujificha tumefurahi sana

Lakini hii sio aina ya furaha tunayoitaka wana Lunyasi

Sisi tunataka furaha yetu ya kutwaa wa Ubingwa wa Afrika

Ni fedheha kubwa sisi kukaa macho usiku kuangalia UTO anacheza fainali

Pamoja na ukweli kwamba njia yao ilikua nyepesi lakini ukweli mwingine ni kwamba wamejua kuitumia iyo njia ya nyepesi

Sisi hua tunapita njia ngumu ni wakati wa kutafuta namna ya kupita kwenye iyo njia ngumu haiwezi kuwa excuse tena eti tumepita njia ngumu

Tumeshamfunga Al Ahly, tushamfunga Wydad nani mwingine mkubwa kabaki jibu ni hakuna kama hakuna kwanini tusichukue huu ubingwa

Imewachukua UTO miaka 30 kufikia rekodi yetu ya kucheza Fainali ya CAF, Sasa tunapaswa kuweka rekodi mpya Afrika

Tunapaswa kuamka ili tuwe wa kwanza kuweka rekodi mpya ambayo UTO atahangaika kuifikia

Kazi kubwa inatakiwa kufanyika ndani na nje ya Uwanja tena ianze sasa

Tunahitaji wachezaji wenye hadhi ya kutupa ubingwa wa Afrika, hadhi ni pamoja na ubora na kujitoa kwa ajili ya timu yetu

SOMA NA HII  BALEKE ATOA AHADI HII LEO DHIDI YA COASTAL UNION...

1 COMMENT