Home Habari za michezo MKATABA MPYA WA ‘BACCA’ YANGA SIO KITOTO….MSHAHARA ATAKAO LIPWA HUU HAPA…

MKATABA MPYA WA ‘BACCA’ YANGA SIO KITOTO….MSHAHARA ATAKAO LIPWA HUU HAPA…

Habari za Yanga SC

RAIS wa klabu ya Yanga, Eng Hersi Ally Said amethibitisha kuwa mlinzi Ibrahim Hamad ‘Bacca’ amesaini nyongeza ya mkataba mpya wa kuendelea kusalia Yanga SC sambamba na nyongeza ya mshahara mkubwa.

Akizungumza kupitia #WasafiFM Eng Hersi Ally Said amesema; “Hii ni Exclusive ambayo naitoa hapa @wasafifm, Ibrahim Bacca Tumemuongezea Mkataba na Mshahara Mkubwaa. Sivwezi kuutaja hapa Kwasababu ni mkataba wa siri wa pande mbili.”

Taarifa kutoka Yanga zinadai kuwa Bacca ameongeza mkataba wa miaka mitatu ambapo pamoja na mambo mengine atakuwa akilipwa Milioni  8 kama mshahara pamoja na kuhakikishia posho.

Aidha, mtoa taarifa wetu amedai kuwa Yanga, itampa beki huyo chaguo la kwanza kwa sasa kwenye kikosi cha Nabi, Usafiri wa maana pamoja na kuboreshewa makazi.

Bacca alitua Yanga kwenye dirisha dogo la usajili mara baada ya ‘kukichafua’ kwenye michuano ya kombe la mapinduzi visiwani Zanzibar akiwa kwenye kikosi cha KMKM.

Aidha, Bacca ambaye pia ni mwajiriiwa wa jeshi la Kikosi Maalumu cha Kuzuia Magendo SMZ, hakupata tu nafasi ya kung’aa na Yanga kutokana na kukuta ushindani wa namba kwenye kikosi hicho.

Hivi Karibuno, kulizuka tetesi za beki huyo kunyemelewa na klabu za Simba na Azam kwa kile kilichodaiwa kuwa ni maslahi kidogo na madahifu ya vipengele kwenye mkataba wake na Yanga.

Wakati mabosi wa klabu hizo wakiendelea kumsumbua ‘Bacca’ na kambi yake, ndipo mabosi wa Yanga walipoanza kumtuliza kwa mipango ya baadye.

Mashabiki wengi wa Yanga, wanamlinganisha mchezaji huyo na aliyekuewa nahodha na beki wao Nadir Haroub ‘Canavaro’ ambaye naye alikuwa akicheza kwa jihadi na maarifa.

Kwa sasa, Bacca ni sehemu ya wachezaji muhimu kwenye kikosi cha Yanga, aambapo mara kadhaa Nabi amekuwa akimwanzisha pamoja na Nahodha Bakari Mwamnyeto .

SOMA NA HII  WAZIR JUNIOR BADO ANAFIKIRIA TUZO YA UFUNGAJI BORA