Home Burudani DIAMOND ‘KUKINUKISHA’ SHEREHE ZA YANGA LEO….KALIPWA MAMILIONI HAYA KWA TUKIO HILO TU..

DIAMOND ‘KUKINUKISHA’ SHEREHE ZA YANGA LEO….KALIPWA MAMILIONI HAYA KWA TUKIO HILO TU..

Habari za Yanga leo

Ikiwa Club ya Young Africans wameandika rekodi nyingine ya kuchukua kombe la Shirikisho la Azam Sports katika fainali iliyochezwa jana Juni 12, 2023 Mkoani Tanga katika Dimba la Mkwakwani baada ya kuibuka kwa ushindi wa goli moja dhidi ya Azam FC.

Sasa Uongozi wa timu hiyo imetangaza rasmi kuwa leo June 13, 2023 kutafanyika shamra shamra za kusherehekea Ubingwa na Mafanikio ya timu yao wa msimu huu huku wakiwataka wanachama, Mashabiki na Wapenzi wa timu hiyo kuungana nao katika viunga majira asubuhi saa tatu Karume- Msimbazi kisha kumalizika katika Makao Makuu ya Young Africans SC Jangwani Dar es Salaam.

Parade hiyo ya Mabingwa wa kihistoria itasindikizwa na msanii na mmiliki wa leo ya WCB, Diamond Platnumz ambae atawaimbia na kuwachezea mashabiki wa Young Africans watakaofika Jangwani Makao Makuu Dar es Salaam.

Hii inakuwa ni mara ya kwanza Diamond kutumbuiza kwenye tukio la Yanga, huku akikumbukwa kufanya tukio kama hilo kwa Simba , kwenye kilele cha Simba Day ya msimu wa 2019/20 ambapo aliingia uwanjani kwa Helkopta.

Inasemekana kuwa viongozi wa Yanga wamemlipa Diamond zaidi ya Milioni 40 huku ukaribu wake na Msemaji wa klabu hiyo Haji Manara ukichagiza ‘Simba’ kukubali kuwepo kwenye shangwe hizo.

Taarifa za ndani kutoka WCB , zinadai kuwa Diamond huenda kwenye ‘Siku ya Mwananchi’ akatunga wimbo maalumu kwa mashabiki wa Yanga na kutumbuiza pia.

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI YA CAF IJUMAA HII...MZANI WAIANGUA SIMBA....ASEC MIMOSAS WANA 'VIMEO' VINGI...