Home Habari za michezo KUHUSU DILI LA WINGA ‘KIMONDO’ KUTOKA CAMERON KUTUA SIMBA LIKO HIVI…

KUHUSU DILI LA WINGA ‘KIMONDO’ KUTOKA CAMERON KUTUA SIMBA LIKO HIVI…

Tetesi za usajili Simba

Inaelezwea kuwa Klabu ya Simba ya Tanzania imefikia makubaliano ya kuinasa saini ya winga anayekipiga Klabu ya Rayon Sports ya Rwanda Leandre Essomba Willy Onana.

Timu hiyo kwa sasa inapambana kusuka upya kikosi hicho na tayari imeshaachana na kiungo Agustino Okra raia wa Ghana ambaye ndani ya ligi alitupia mabao manne.

Simba inahitaji kuvunja rekodi ya Yanga kucheza fainali Kombe la Shirikisho na hesabu zao ni kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

Onana ni raia wa Cameron anatajwa kubiukia ndani ya kikosi hicho kwa msimu ujao wa 2023/24.

Nyota huyo mwenye miaka 23 inaelezwa kuwa amekataa kujiunga na Singida Big Stars baada ya ofa ya Simba kuwa nzuri.

Kwa 2022/23 ni kinara wa ufungaji mabao kwenye ligi ya Rwanda baada ya kufunga mabao 16 na kutoa assists 10.

SOMA NA HII  JEZI YA MTANZANIA YAUZWA UBELGIJI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here