Home Azam FC AZAM FC WAFANYA KWELI KWA FEI TOTO…WAIPA YANGA MIL 270….MSHAHARA ATAKOLIPWA HUU...

AZAM FC WAFANYA KWELI KWA FEI TOTO…WAIPA YANGA MIL 270….MSHAHARA ATAKOLIPWA HUU HAPA…

Tetesi za Usajili

BAADA ya mgogoro wa muda mrefu kati ya Klabu ya Yanga na mchezaji wao Feisal Salum ‘Feitoto’ ni rasmi sasa wamemaliza mgogoro huo na kumuuza kwenda Azam FC.

Taarifa hiyo imetolewa leo kupitia Idara ya Habari na Mawasiliano ya mitandao ya kijamii ya klabu hiyo na kueleza kuwa uamuzi huo umefikiwa baada ya makubaliano ya pande zote mbili.

Taarifa imeeleza kuwa Feisal ameuzwa kwa dau ambalo halitawekwa wazi kutokana na makubaliano ya pande zote mbili.

“Uongozi wa Yanga unapenda kuutarifu umma kuwa umepokea ofa kutoka katika klabu ya Azam FC ya kumuhitaji Feisal Salum na baada ya makubaliano ya pande zote mbili uongozi umefikia uamuzi wa kumuuza mchezaji huyo kwa klabu ya Azam FC,” ilieleza taarifa hiyo

Taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo zinasema kuwa Yanga wamemuuza kwa dau la Mil 270 kiungo huyo pesa ambazo ziitalipwa kwa awamu mbili, ambapo kwanza wakianza na mil 150.

Inaelezwa kuwa Azam na Fei Toto walishamalizana kitambo toka sakata lake na Yanga kuibuka, ambapo duru za michezo nchini zinadai kuwa Kiungo huyo atalipwa mshahara wa Mil 16 kwa mwezi.

Mbali na mshahara huo, Familia ya Fei Toto watapewa nyumba Zanzibar, huku mchezaji huyo akipewa gari ya kisasa ya kutembelea na kupewa nyumba ya kuishi Dar.

Yanga wameafikia kumuuza Fei Toto baada ya Rais Samia Suluh kuwataka walimalize sakata hilo juzi Ikulu , kwenye dhifa ya kitaifa aliyowaandalia.

Katika ombi lake kwenda kwa Rais wa Yanga, Rais Samia aliwataka kulimaliza suala hilo haraka , kwani haipendezi klabu kubwa kama Yanga kuwa na misukosuko na wachezaji.

Sakata la Fei Toto na Yanga lilianza mwanzoni mwa mwaka huu, ambapo mchezaji huyo alidai kuwa halipwi kulingana na mchango anaoutoa kwenye klabu hiyo.

SOMA NA HII  BAADA YA KUIBANJUA KMC JANA....NABI HATAKI MASIKHARA YANGA....MORRISON NA WENZAKE 'WATEMESHWA NYONGO'...