Home news LIGI YA WANAWAKE WAPEWA USHAURI HUU WA BURE

LIGI YA WANAWAKE WAPEWA USHAURI HUU WA BURE

Kocha maarufu wa Soka la Wanawake aliyewahi kuzinoa Simba Queens na Yanga Princess, Sebastian Nkoma ameshtukia jambo kwenye Ligi Kuu ya Wanawake (WPL) kisha kuziuma sikio klabu zinazoshiriki ligi hiyo.

Nkoma anatajwa kuwa mbioni kurejea Msimbazi kuinoa tena Simba Queens kwa msimu ujao wa WPL na michuano ya kimataifa, baada ya kuondolewa Septemba mwaka jana baada ya kuipa timu hiyo ubingwa wa CECAFA na kukata tiketi ya kushiriki Klabu Bingwa Afrika na kufika nusu fainali.

Kocha huyo aliyenyakuliwa na Yanga Princess Desemba 10 mwaka jana kuchukua nafasi ya Edna Lema, kabla ya kuachana nayo Machi mwaka huu amesema ili timu zifanikiwe katika WPL msimu ujao ni lazima zifanye usajili wa kueleweka pamoja na kuweka malengo kabla ya kivumbi hakijaanza.

Nkoma alisema timu nyingi za WPL zinafanya mambo kwa mazoea kama zimejikuta tu zikicheza ligi hiyo, hivyo ni lazima zianze kujipanga mapema.

“Kitu cha muhimu ni kufanya usajili kwani wachezaji wa kike ni wachache, lakini pia kuweka malengo ya kipi cha kufanya sio kitu cha kuupuuzwa. alisema Nkoma.

SOMA NA HII  MASTAA HAWA UANGA WAITAMANI SIMBA KUFA KUPONA DABI YA KARIAKOO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here