Home Habari za michezo KOCHA MPYA YANGA AMALIZA UTATA ISHU YA LOMALISA…AKOSOA NABI ALIVYOKUWA AKIMTUMIA..

KOCHA MPYA YANGA AMALIZA UTATA ISHU YA LOMALISA…AKOSOA NABI ALIVYOKUWA AKIMTUMIA..

Habari za Yanga SC

Sikia hii. Kama ulikuwa unadhani zile ‘Thank You’ walizopewa mastaa wa Yanga zimeshakamilika, basi utakuwa umekosea sana, kwani kuna jipya linatarajiwa kupitishwa tena na kocha mkuu mpya, Miguel Angel Gamondi kufyeka baadhi ya nyota watakaoshtua mashabiki wa klabu hiyo.

Kocha huyo kutoka Argentina anaonyesha hatanii kwani mipango yake ni kusuka kikosi cha kisasa zaidi na juzi amewashtua mabosi wa klabu yake akiwatangazia kwamba anataka kuona kikosi chake kinacheza soka la kisasa litakalohusisha mipango ya kisasa ya kuzuia, ila akili kubwa ni kushambulia.

Inafahamika kuwa beki mwenye maana ambaye amepitishwa haraka na Gamondi ni Joyce Lomalisa Mutambala ambaye amezuia Mkongomani huyu kuondoka akitaka amkute kwani anajua matumizi yake katika kikosi hicho.

“Tulimueleza Lomalisa anataka kuondoka, akaangalia jinsi alivyocheza msimu uliopita, akasema alikuwa anakosewa matumizi yake, akatuambia tumwambie abaki anakuja kufanya naye kazi,”

Bosi huyo aliongeza “Hivyo kuna watu zaidi wanaweza kuja kukatwa watakaoshtua lakini ndio kocha ametaka, anachotaka ni kuona anabaki na watu ambao watakuwa na namba nzuri za kumpa matokeo, ametuambia maamuzi yake hayataangalia jina la mchezaji, akitolea mfano mtu kama Mayele (Fiston) akisema ameridhishwa sana na kazi kubwa aliyoifanya.”

SOMA NA HII  PAMOJA NA KUSAJILIWA NA WAARABU JUZI JUZI.....RONALDO AJIRUDISHA MADRID KIAINA...