Home Habari za michezo WAKATI MASHABIKI WAKISUBIRI ‘THANK YOU’ YA ONYANGO…AHMED ALLY KAAANIKA JAMBO LILIVYO…

WAKATI MASHABIKI WAKISUBIRI ‘THANK YOU’ YA ONYANGO…AHMED ALLY KAAANIKA JAMBO LILIVYO…

Tetesi za Usajili Simba

Uongozi wa Simba SC umetangaza kuwa beki wao kutoka nchini Kenya, Joash Onyango Achieng, bado mali halali ya klabu hiyo, licha ya mkataba wake kubaki mwaka mmoja, huku mara kadhaa ikiripotiwa kwamba ameandika barua ya kusitisha mkataba wake huo.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, amesema Onyango bado ataendelea kubaki Simba kwa msimu ujao.

Ameongeza kuwa bado beki huyo anahitajika katika timu hiyo, kutokana na ubora alionao wakati wakijiandaa na michuano ya kimataifa msimu ujao 2023/24.

β€œHicho kinachoendelea na uvumi tu, hakuna barua yoyote tuliyoipokea kutoka kwa Onyango ya kuomba kuondoka.

β€œWatu wafahamu kuwa Onyango ni mchezaji halali wa Simba SC ambaye mkataba wake unatarajiwa kumalizika msimu ujao,’ amesema Ahmed Ally.

SOMA NA HII  HAJI MANARA ANUSURIKA NA AJALI MBAYA YA GARI USIKU...AFUNGUKA HAYA..