Home Habari za michezo AMRI KIEMBA AMKINGIA KIFUA SALIM ALLY, ASEMA HAYA KUHUSU SAKATA LA PENATI...

AMRI KIEMBA AMKINGIA KIFUA SALIM ALLY, ASEMA HAYA KUHUSU SAKATA LA PENATI DHIDI YA YANGA

kiemba

Mchezaji wa zamani wa Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars na Mchambuzi wa michezo kupitia kituo cha Clouds Media Amri Kiemba amewataka Mashabiki na wapenda Soka nchini kujitokeza na kumpongeza mlinda mlango wa Simba SC Ally Salim baada ya kuiwezesha Simba kutwaa Ngao ya Jamii 2023.

Mchezo huo uliopigwa Agosti 13 katika Dimba la CCM Mkwakwani Jijini Tanga uliwashuhudia Simba wakibeba Kombe la kwanza baada ya misimu miwili kutoka kapa.

Sasa kitendo cha Ally Salim kuokoa penati tatu za Yanga wengi wamepiga kelele kuwa Golikipa huyo alitoka kwenye eneo lake kabla ya mpira kupigwa.

Kiemba anasema;

“Watu wote wameanza kusema ametokea ndio amedaka lakini makipa huwa wanatoka na wanafungwa ,sheria inasema akitoka ukafunga ni goli kwa hiyo Ally Salim kutokea na kudaka anapaswa kusifiwa”

“Ile sio mara ya kwanza kudaka penati alisave penati mechi ya Singida na hata aliyofungwa na Aziz Ki aliifuata”

SOMA NA HII  ZA NDANI KABISA...VIGOGO YANGA WAMPA MAISHA YA KIFAHARI PRINCE DUBE...ISHU NZIMA IPO HIVI