Home Habari za michezo BAADA YA KUANZA VIBAYA NYONI AFUNGUKA MIPANGO YA NAMUNGO

BAADA YA KUANZA VIBAYA NYONI AFUNGUKA MIPANGO YA NAMUNGO

Kiungo wa Namungo FC, Erasto Nyoni amesema licha ya kuanza vibaya michezo yao ya Ligi Kuu Tanzania Bara lakini anaamini watafanya vizuri msimu huu 2023/24.

Kiungo huyo amesema kinachompa imani hiyo ni aina ya wachezaji waliosajiliwa na timu hiyo na uzoefu waliokuwa nao.

Timu yetu ina wachezaji wengi wenye uzoefu na ligi, lakini pia hata benchi letu la ufundi lipo vizuri ndio maana matumaini ya Namungo kufanya vizuri msimu huu kwangu ni makubwa,” amesema Nyoni.

Mkongwe huyo aliyewahi kutamba na miamba ya soka nchini Simba SC, amesema baada ya kupata pointi moja kwenye mechi tatu walizocheza za ligi mpango wao ni kuhakikisha wanashinda mechi zinazofuata.

Nyoni amesema yeye na wachezaji wenzake wamejipanga kuhakikisha wanabadilisha matokeo mabaya na kupata ushindi ambao utatimiza malengo ambayo wamedhamiria kuyafikia msimu huu.

Malengo ya Namungo FC msimu huu ni kumaliza ligi kwenye nafasi tatu za juu ili kupata nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa msimu ujao 2024/25.

SOMA NA HII  MZIMU WA MAYELE WAENDELEA KUSAKAMA YANGA, KUMPATA MRITHI WAKE MAJANGA, MPOLE AHUSISHWA