Home Habari za michezo HAYO MAANDALIZI YA GAMONDI DHIDI YA AL MAREIKH SIO POA

HAYO MAANDALIZI YA GAMONDI DHIDI YA AL MAREIKH SIO POA

Habari za Yanga SC

KUELEKEA mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Yanga dhidi ya Al Merrikh, Waarabu hao wa Sudan watakutana na balaa jipya linalosukwa na Miguel Gamondi ambaye ni Kocha Mkuu wa Yanga.

Mchezo huo unaotarajiwa kuchezwa Septemba 30, mwaka huu kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar, utatoa mshindi wa jumla atakayekata tiketi ya kutinga hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika.

Akizungumza na Spoti Xtra, Gamondi alisema kila mchezo una mbinu tofauti kulingana na aina ya wapinzani jambo linalofanya wabadili mara kwa mara.

“Kila mchezo una mbinu zake kulingana na aina ya wapinzani tunaokutana nao, tunachohitaji ni kupata ushindi na kuelekea mchezo wetu tutakaokuwa Dar dhidi ya Al Merrikh tutakuwa na maandalizi mazuri ambayo yatatupa matokeo bora.

“Wachezaji wapo tayari kwa ajili ya kupata matokeo mazuri. Tunaongea nao kwenye uwanja wa mazoezi namna ya kufanya katika kupunguza makosa na kutumia makosa ya wapinzani kupata matokeo mazuri,” alisema Gamondi.

Katika mchezo wa kwanza uliochezwa Rwanda, Yanga ilishinda mabao 0-2, watupiaji wakiwa ni Kennedy Musonda na Clement Mzize.

SOMA NA HII  KAMWE:- WAARABU TUMEWASOMA...TUMEWAPIGIA MAHESABU MAKALI...WATASHANGAA MPIRA BOLIBO

1 COMMENT