Home Habari za michezo MASTAA HAWA WA SOKA BONGO KAMA ULAYA

MASTAA HAWA WA SOKA BONGO KAMA ULAYA

Habari za Yanga SC

Mara nyingi wakati wa mapumziko tumezoea kuona wachezaji wanao cheza soka la kulipwa ulaya wakati wa mapumziko wakioneka katika viwanja vikubwa kufatilia mchezo wa Basket ball hasa nchini Marekani.

Hata hapa Tanzania nyota wa mpira wa miguu kutoka vilabu vya Yanga SC na Azam FC Skudu Makudubela pamoja na Aziz Ki na kwa upande wa Azam FC Idd Seleman Nado wameonekana katika uwanja wa Don Bosco Oysterbay kwenye fainali za ligi ya kikapu BD League Skudu na Nado wamefunguka na kueleza kwanini wamekwensa kutazama Mpira wa kikapu.

“Michezo ni kitu ambacho kinagusa hisia za watu kwahiyo hata Mimi mchezo huu umenigusa na nime shawishika kuja kutazama Mpira huu nime enjoy sana”Amesema Skudu

“Ni mefurahi kuwa hapa ni mara ya kwanza kuja kutazama ni mchezo ninao upenda pia nikipata nafasi nikiwa mapumziko nitakuwa nakuja kutazama zaidi maana tunaona hata wachezaji wa ulaya wanapenda kutazama mchezo wa basket”Alisema Idd Nado

SOMA NA HII  NAMUNGO: TUMEPATA FUNZO