Home Habari za michezo MUDATHIR:- BAO LILIANZIA BENCHI…

MUDATHIR:- BAO LILIANZIA BENCHI…

Yanga vs Namungo

Bao pekee lililofungwa na Mudathir Yahya katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Namungo FC limeifanya Yanga SC kuongoza katika msimamo wa ligi hiyo wakifikisha pointi tisa.

Katika mechi hiyo iliyopigwa jana Jumatano, Septemba 20, 2023 katika Dimba la Azam Complex, Chamazi Dar, Mudathir alifunga bao hilo dakika ya 88, baada ya kuingia kipindi cha pili kuchukuwa nafasi ya Pacome Zouzoua.

Akizungumzia maelekezo aliyopewa na kocha wake, Miguel Gamondi kabla ya kuingia uwanjani, Mudathir amesema;

“Azam Complex nimeingia kwenye kiwanja changu, Kocha aliniambia ‘watu wamekaa nyuma wote, ukiona mpira unakwenda pembeni ni kitu ambacho tunakifanya kwenye mazoezi kila siku, kimbia nyuma ya mabeki.’ Nimekimbia nyuma ya mabeki na nikakutana na mpira nikaweka kambani.

“Hakuna mchezo mgumu kama watu kukaa nyuma tu, wameweka basi nyuma wakipata wao wanatupa sisi tucheze ndiyo maana ukaona tumepata nafasi nyingi tumeshindwa kuzitumia. Tungezitumia zile nafasi zingefika zile goli zetu (5), lakini haikuwa bahati yetu, tumepata nafasi moja tukafunga, tunamshukuru Mwenyezi Mungu.

“Nikiwa benchi nilikuwa nawaza kuipa ushindi timu yangu sababu kila tukipata ushindi timu yetu inakuwa juu na wachezaji tunaheshimika.

“Kwenye mapumziko mwalimu alisema namungo wamekuja aggressive, na sisi tuingie aggressive, kwenye 50/50, watu wakafuata maelekezo,” amesema Mudathir.

SOMA NA HII  KUHUSU MSIMU UJAO NA UHAKIKA WAKE WA KUBAKI....BANGALA AMTAJA KWANZA IBENGE...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here